NUKUU ZA WIKI

Nyerere: Kujitolea muhimu kwenye chama

“Lakini chama chochote, hata chama cha michezo tu, lazima kiendeshwe na mashabiki kwa njia za kujitolea. Moyo wa kujitolea ukifa, chama hakiwi chama tena; kinakuwa ni chaka tu la mawindo ya kujitafutia mali.”

Maneno haya ni maneno ya Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Teresa: Watu wanakuja kama Baraka, masomo

“Baadhi ya watu wanakuja katika maisha yako kama Baraka. Baadhi wanakuja katika maisha yako kama masomo.”

Haya yalisema na Mtawa wa Kanisa Katoliki wa nchini India, Mother Teresa. Alizaliwa Agosti 26, 1910, alifariki Septemba 5, 1997.

 

Mchechu: Ninakerwa Tanzania kuitwa maskini

“Maelezo kwamba Tanzania ni nchi maskini yananikera. Imefika mahala wanasiasa wanadhani ili uwe kiongozi bora lazima ujiainishe kuwa unatetea umaskini.”

Haya ni maneno ya Mkiurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu.

 

Mandela: Kuna milima mingi ya kupanda

“Baada ya kupanda mlima mmoja wa nguvu, unakuta kuna milima mingine mingi ya kupanda.”

Kauli hii ilitolewa na Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Alikuwa akiwakumbusha wananchi wake kuwa uhuru si mwisho wa matatizo.