Nyerere: Vyama viwasaidie wananchi kujiendeleza

“Lazima chama [cha siasa] kiwasaidie wananchi kujiendeleza na kupanua mawazo yao kwa kuwaelimisha, kwa kuwaunganisha kwa hiari katika shughuli zao za kujitegemea, na kadhalika.”

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Geun-hye: Nitaijenga nchi yenye watu wanaoshiba

“Uchumi wa Korea Kusini bado ni mgumu. Nitaijenga nchi ambayo hakuna mtu atakayekuwa na wasiwasi kuhusu kutenga chakula mezani.”

Hii ni kauli ya Rais Geun-hye Park wa Korea Kusini. Ndiye mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais nchini humo.

 

Mandela: Kiongozi huwa mstari wa mbele vitani

“Kiongozi mzuri ni yule anayesimama nyuma wakati wa sherehe za ushindi, na ambaye anakuwa mstari wa mbele wakati wa matatizo na vita.”

Maneno haya ni ya kiongozi wa ukombozi wa Afrika Kusini kutoka katika udhalimu wa Makaburu, Rais mstaafu Nelson Mandela.

 

Abramson: Najiona mwandishi mbabe, sio mtu mbabe

“Nafikiri mimi kama mwandishi wa habari za uchunguzi nina ubabe wa viwango, lakini sifikiri kama mimi ni mtu mbabe.”

Kauli hii ni ya Jill Abramson, Mhariri Mtendaji wa gazeti maarufu linaloitwa New York Times la nchini Marekani.

 

 

 

1412 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!