Julius Nyerere: Kumteta mtu ni kumdhuru

“Wengine humwona mwenzao anafanya kosa, badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ndiye Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.

Angela Merkel: Wanasiasa waongoze kwa usawa

“Wanasiasa wanapaswa kuwajibika kwa kuwatumikia watu kwa kipimo kilicho sawa. Linapokuja suala la utu wa mtu hatuwezi kufanya maafikiano.”

Haya yalinenwa na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel. Ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini humo.

 

David Cameron: Mifumo siasa, uhumi imevunjwa

“Mfumo wa kisiasa umevunjwa, uchumi umevunjwa na hiyo ndiyo jamii. Hiyo ndiyo sababu ya watu kuhuzunika sana kuhusu hali ya nchi yetu [Uingereza].”

Kauli hii ni ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David William Donald Kameron, ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha Conservative na Mbunge wa Witney nchini humo.

 

Susan Wojcicki: Google inatumiwa na wengi

“Watu katika hatua tofauti za maisha yao wanafanya vitu tofauti, na wote wanatumia Google. Ninawajibika kutengeneza na kusimamia bidhaa za baadaye zinazoinua matangazo ya Google.”

Haya ni maneno ya Mwanamke mfanyabiashara maarufu wa nchini Marekani, Susan Wojcicki, ambaye pia ni Makamu Mwandamizi wa Rais wa Kampuni ya Google.

1211 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!