Julius Nyerere: Kujidai unajua kila kitu ni hatari

“Kiongozi anayejidai kuwa anajua kila kitu, na kumbe hajui, ni hatari zaidi kuliko yule anayekiri kuwa hajui kitu na yuko tayari kujifunza.”

 

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Alizaliwa 1922, akafariki 1999.

 

Alice Walton: Nasimamia mali kuongeza thamani

“Moja ya majukumu makubwa niliyo nayo ni kusimamia mali zangu, ili ziweze kuongeza thamani.”

 

Kauli hii ni ya Alice Louise Walton wa Marekani, ambaye ni tajiri anayeshika nafasi ya tatu duniani kwa upande wa wanawake. Alizaliwa Oktoba 1949.

 

Dk. Salim: Katiba izingatie matakwa ya umma

“Katiba mpya lazima izingatie matakwa ya wananchi. Tunapaswa kuepuka maslahi binafsi ili kuunda Katiba itakayonufaisha umma kwa jumla.”

 

Haya yalisemwa na Dk. Salim Ahmed Salim aliyepata kuwa Katibu Mkuu wa OAU na Waziri Mkuu wa Tanzania.

 

Dk. Ndalichako: Taaluma isiingiliwe na kila mtu

“Wanaotunga sheria watekeleze jukumu lao, wasiingilie moja kwa moja suala la mitihani. Sisemi kuwa tuachwe tu tufanye kazi kama tunavyotaka, ikibidi kuwe na chombo cha wanataaluma kutukagua, kwa sababu hii ni taaluma siyo kitu cha kila mtu kuingilia.”

 

Hii ni kauli ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako.

 

By Jamhuri