Mwalimu Nyerere: Tudhibiti tofauti za maskini, matajiri

“Tofauti kati ya watu maskini na watu matajiri zinaongezeka Tanzania. Inafaa tuwe macho. …lazima tuendelee kutumia Sheria za Nchi, na mipango mbalimbali ya Serikali, kuona kuwa tofauti hizi hazifikii kiasi cha kuhatarisha umoja na amani.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bill Gates: Epuka kujilinganisha na wengine

“Usijilinganishe na mtu yeyote katika dunia hii… Kama unafanya hivyo, unajitukana wewe mwenyewe.”

Hii ni kauli ya mfanyabiashara maarufu na bilionea wa nchini Marekani, William Henry “Bill” Gates.

Stephen Wasira:

“Hati ya Muungano ni document nyeti sana, huwezi kuachia wajumbe waishike, badala yake wataonyeshwa. Unaweza kumpa mjumbe mwingine bila kutarajia akaichana na kuleta shida kubwa sana, kwa sababu wapo wajumbe wasiotaka kusikia Muungano.”

Kauli hii ni ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, anayeshughulikia masuala ya Uhusiano na Uratibu Tanzania, Stephen Masato Wasira.

Maya Angelou:

“Kama hupendi kitu fulani, kibadilishe. Kama huwezi kukibadilisha, badilisha tabia yako.”

Matamshi haya ni ya mtunzi maarufu wa mashairi wa nchini Marekani, Maya Angelou.

2397 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!