“Kupima utajiri wa taifa kwa kutumia vigezo vya pato la taifa ni kupima vitu, si ufanisi.”

Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa Januari 2, 1973 jijini Khartoum, Sudan katika mkutano wa kuimarisha pato la taifa kwa nchi za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara.

Powell: Kiongozi hakati tamaa

“Hata kama umepata maswahibu au la, jukumu la kiongozi ni wakati wote kuonesha moyo wa ushindi.”

Haya ni maneno ya aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Colin Powell, wakati akichagiza Wamarekani kuendeleza vita dhidi ya Iraq.

 

Dalai Lama: Utu Kwanza

“Chimbuko letu ni utu, si kiongozi huyu, kiongozi yule au mfalme au mtoto wa mfalme au kiongozi wa kidini. Dunia chimbuko lake ni utu.”

Haya ni maneno ya kiongozi wa Watibeti wapigania uhuru wa Jimbo la Myanmar, Dalai Lama, akiwahamasisha wenzake kutoogopa binadamu wenzao katika mapambano ya haki.

 

Nixon: Kiongozi mtata muhimu

“Kama mtu anataka kuwa kiongozi na hajawahi kukwaruzana na yeyote [akimfurahisha kila mtu], fahamu  kuwa hajapata kusimamia jambo lolote [la maana lenye kuleta utata].”

Haya ni maneno ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Richard Nixon, wakati akiwaambia wananchi wa Marekani kuwa kiongozi anayesulubiwa ni yule aliyesimamia ajenda yenye ufanisi akawakera wenzake kwa mafaniko aliyopata.

By Jamhuri