LISOME GAZETI LETU LA JAMHURI LA KILA WIKI HAPA

Habari Mpya

January Makamba amefanya jambo la kuigwa

Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba, ametangaza kuwa amejipanga kuongeza kasi ya maendeleo ya elimu katika jimbo hilo, kazi itakayofanyika kwa kupitia Shirika la Maendeleo Bumbuli (BDC) kuanzia mwaka huu.

 

Programu hiyo itagharimu Sh. milioni 40 ikijumuisha vivutio kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari; yote ikilenga kuongeza tija na umakini wa kujifunza na kusaidia juhudi zinazofanywa na serikali katika elimu.

Read More »

Ardhi ya Tanzania inavyoporwa na matajiri matapeli

*Kambi ya Upinzani yaanika bungeni uozo wa kutisha

*Familia ya Chavda yavuna mabilioni na kutokomea

 

Hii ni sehemu ya hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee, aliyoitoa bungeni wiki iliyopita, akieleza namna ardhi ya Tanzania inavyohodhiwa na wafanyabiashara na matajiri matapeli…


MASHAMBA YALIYOBINAFSISHWA AMBAYO HAYAJAENDELEZWA

Mheshimiwa Spika, wakati akihitimisha bajeti ya ardhi mwaka jana, Waziri wa Ardhi aliliahidi Bunge lako Tukufu kwamba baada ya Bunge la bajeti wizara ingekwenda kufanya ukaguzi huru wa nani ametelekeza mashamba. Alisisitiza kwamba wawekezaji wote waliotelekeza mashamba “the honeymoon is over.”

Read More »

‘Majaji ndiyo waliomtuma Lissu’

Hotuba kali ya Tundu Lissu ya kukosoa uteuzi wa majaji dhaifu uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete, imeelezwa kwamba ina baraka zote za baadhi ya viongozi waandamizi wa Mhimili wa Mahakama, JAMHURI limeelezwa.

Read More »

Wapinzani wachekelea Pinda kugwaya

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kufarijika na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba kampuni ya Agrisol haijapewa ardhi ya Katumba na Mishamo mkoani Katavi.

Read More »

Tuwe makini kulinda ardhi yetu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, jana aliwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo ya mwaka 2012/2013.

Read More »

Sasa umefika wakati wa vitendo-Tibaijuka

[caption id="attachment_195" align="alignleft" width="160"]Profesa Anna Tibaijuka[/caption]Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuanzia sasa inachofanya ni vitendo tu katika kukabiliana na wavunjifu wa sheria za ardhi, wakiwamo wavamizi wa maeneo yasiyoruhusiwa kujengwa.

Read More »

Sinema kwa wasioona zaja

  Badala ya utaratibu wa zamani sasa waonyesha sinema wamebuni utaratibu mpya wenye kuwawezesha watu wasioona kuangalia sinema sambamba na watu wanaoona.   Teknolojia hii ...

Read More »

Brigedia Jenerali aliasa Taifa (2)

Pamoja na malalamiko mengi na ya mara kwa mara, lakini ndugu zangu Watanzania wenzangu hawa wamejaaliwa uwezo mkubwa sana kiuchumi (have a very strong economic base). Hilo kamwe hawalitangazi wanaliacha kwenye “low profile”- mambo yao kimya kimya tu.

 

Read More »

Habari za Kitaifa

Maoni ya Mhariri

Nyundo ya Wiki