KATIBU  wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema Askofu Zakaria Kakobe  na viongozi wengine wa dini  hawajazuiwa kuongea na kwamba wako huru kutoa maoni yao.

Polepole ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni  na kusema kuwa hakuna mtu ambaye ametishwa kwa kusema ukweli juu ya jambo fulani ambalo huenda lipo au linatokea Tanzania.

Polepole amesema kuwa Hakuna mtu amezuiliwa kuongea ukweli Tanzania, wala kutishwa kwa kusema ukweli na hasa katika uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika hatua nyingine kamanda wa polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa. amekanusha taarifa kuwa Jeshi hilo linamshikilia Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Bible fellowship Zakari Kakobe kwa tuhuma za uchochezi.

Alhamis wiki hii Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Mst. Projest Rwegasira, ilitoa onyo kwa viongozi wa jumuiya za kidini kutotumia mahubiri yao ya ibada kwa kufanya uchambuzi wa masuala ya siasa.

By Jamhuri