Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation – NHC) Bi. Blandina Nyoni kuanzia leo tarehe 21 Machi, 2018.

Pia Mhe. Rais Magufuli ameivunja Bodi ya NHC kuanzia leo.

Uteuzi wa Mwenyekiti na bodi nyingine utafanyika baadaye.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

21 Machi, 2018

1693 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!