Real Madrid kuivua ubingwa Bayern leo

Miamba minne ya soka barani Ulaya, wiki hii inajitupa tena katika viwanja viwili tofauti kucheza nusu fainali ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).
Miamba hiyo ni mabingwa watetezi wa kombe hilo, vijana wa Pep Guardiola wa Bayern Munich, watawakaribisha vijana wa Carlo Ancelotti wa Real Madrid pale Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani.
Wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kuwa mchezo huo ni sawa na fainali kwani Bayern Munich inatakiwa kushinda mchezo huo ili kutetea ubingwa wake.
Katika mechi iliyopita, Real Madrid ilishinda kwa bao 1-0 na kujiwekea akiba nzuri kibindoni itakayowapa nafasi ya kuendelea kampeni yake ya kuwania kuivua ubingwa wa Bayern.
Karim Benzema ndiye aliyetingisha wavu wa Bayern mapema katika kipindi cha kwanza.
Mashambulizi ya Cristiano Ronaldo yalikuwa yakisisimua lakini hayakuzaa matunda zaidi kwa Real. Juhudi za Bayern za kurudisha bao hilo zilizimwa.  Hatua hiyo imeifanya Real kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa nyumbani kufikia mechi 18.
Bayern sasa inatakiwa kutumia nderemo, vifijo na mitetemeko ushangiliaji za mashabiki wake ili kuishinda Real Madrid. Mshindi kati ya Bayern na Madrid  atakutana na Chelsea au Atletico Madrid, kutokana na matokeo ya mechi ya kesho.
Je, kelele za ushangiliaji wa mashabiki wa soka wa Bayern Munich zitaweza kuwazuia washambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, Cristiano Ronaldo na Jesé Rodríguez?
Hata hivyo, mabingwa hao mara tatu wa Kombe hilo la Ulaya na mabingwa mara 19 wa Kombe la Ujerumani  wakiongozwa  Pierre-Emile Hojbjerg, Toni Kroos, Mario Mandzukic, Claudio Pizarro na Patrick Weihrauch.
Wengine ni Manuel Neuer, Tom Starke, Lukas Raeder, Patrick Weihrauch, Thomas Müller, mtoto wa gwiji la soka la Ujerumani, Gerd Muller, aliyeshiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1966, Lukas Raeder, Dante, Daniel van Buyten na Rafinha, wakati Diego Contento, Holger Badstuber, Thiago, Frank Ribéry na  Javier Martínez, wakiibeba timu yao.
Wachezaji hao wenye kasi na pasi za uhakika, hawatakuwa tayari kuona Real Madrid wakitibua mbinu zao za kuwania ubingwa katika ardhi ya Ujerumani.
Mechi nyingine itachezwa kesho wakati vijana wa Jose Mourinho, iliyoanzishwa mwaka 1905 na kuja kuwa bingwa wa England baada ya miaka 50 na yenye maskani yake katika mji wa Fulham, jiji la London, itakapowakaribisha vijana wa Diego Simeone, Atletico Madrid katika uwanja wa Stamford Bridge.
Katika raundi ya kwanza ya mchuano wa nusu fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya kati ya Chelsea ya Uingereza na Atletico Madrid ya Uhispania, zilitoka sare ya bila kufungana.
Chelsea ikicheza ugenini tangu mwanzo ilionekana kwamba inahitaji sare kutokana na kulinda zaidi lango lake kuliko kushambulia. Vijana wa Atletico Madrid ambao msimu huu ni moto wa kuotea mbali, walipata nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia.
Chelsea ilipata pigo katika dakika za awali baada ya mlinda mlango wake, Petr Cech, kuumia. Aidha katika dakika za mwisho nahodha wa Chelsea, John Terry, naye aliumia na kulazimika kutoka nje.
Kwa matokeo hayo Chelsea imejiweka katika mazingira mazuri kwenye mechi ya marudiano wakati itakapokuwa mwenyeji.
Mechi nyingine ya kwanza ya nusu fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya inafanyika leo kati ya mabingwa watetezi Bayern Munich na Real Madrid. Mechi hiyo itapigwa katika uwanja wa nyumbani wa Real Madrid wa Santiago Bernabeu.