Mchezaji mpya aliyesajiliwa Simba, Adam Salamba, leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC katika mashindano ya SportPesa Super Cup mjini Nakuru, Kenya.

Salamba alishindwa kujiunga na Simba tangu mwanzo wa mashindano kutokana na kuelezwa kuwa alikuwa anakabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Jana usiku mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka Lipuli na kusaini mkataba wa miaka miwili, aliwasili mjini Nakuru kuungana na wenzake kambini.

Baada ya kuonesha kiwango chake mahiri ndani ya Lipuli msimu uliopita, wadaau na mashabiki wa soka wanatarajia kuona kipi atakionesha pia leo kwenye timu yake mpya.

Simba itakuwa inacheza na Kakamega katika hatua ya nusu fainali kuanzia saa 7 kamili za mchana wa leo kwenye Uwanja wa Afraha.

3235 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!