Simba SC imeendelea kujikita kileleni katika Ligi Kuu Bara baada ya kuitandika Mtibwa Sugar  bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mchezo huo uliokuwa unaambatana na mvua iliyokuwa ikinyesha Uwanjani, ulishuhudiwa nyavu zikitikiswa mnamo dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza na Emmanuel Okwi.

Okwi alifunga bao hilo akimalizia kazi mpira wa kichwa kutoka kwa John Bocco na kufanya mchezo huo udumu kwa dakika zote 90 huku matokeo yakisalia 1-0.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuendelea kuonoza ligi kwa kufikisha alama 52 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga wenye 46 mpaka sasa.

Mechi inayofuatia kwa Simba itakuwa dhidi yaTanzania Prisons, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

By Jamhuri