Snake Junior ndio kama mlivyosikia

Wakati mashabiki wa ngumi wakisubiri pambano la kukata na shoka kati ya mabondia mahiri duniani, Manny ‘Pacman’ Pacquiao na Floyd Mayweather, mambo yamekuwa mabaya kwa bondia kinda wa Tanzania, Mohammed ‘Snake Jr’ Matumla.
Snake Junior-mtoto wa bondia mahiri wa zamani wa Tanzania, Rashid ‘Snakeman’ Matumla, alikuwa na ahadi ya kucheza pambano la utangulizi katika uliongo ulipangwa kutumiwa na akina Pacman hapo Mei 2, mwaka huu.


Ahadi yake ilitokana kumchapa mpinzani wake kutoka China, Wang Xin Hua katika pambano la kuwania Ubingwa wa Dunia wa WBF lililofanyika Machi 27, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, taarifa mpya zinasema kwamba Mohammed hatakwenda na tayari chipukizi ameanza kulalamika kwamba waratibu wanamwangusha, “eti wamemtapeli.”


Lakini Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa (PST), Antony Ruta anasema, “Kweli tulipata nafasi ya Matumla kwenda kuzipiga katika ulingo mmoja na Pacquiao na Mayweather, lakini kumekuwa na mabadiliko kutokana na Shirika la ngumi duniani (WBO).
“Walituambia wanataka tumpeleke bondia mwenye uzito wa (55) Bantam, lakini sasa Matumla yeye ana uzito wa (57) Feather Weight…


“…Kutokana na hilo tuliwaomba watuvumilie ili Matumla afanye mazoezi na kupungua ili aweze kufikia uzito huo walioutaka wao, lakini hadi anapigana na yule Mchina alikuwa bado hajafikishwa uzito huo.”
Anasema kutokana na hali hiyo, waliandika barua kutoa lakini kabla ya majibu wakaambiwa nafasi imejazwa na bondia kutoka Morocco, Said El Harrack.
“Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa, lakini tunashangazwa na maneno ambayo tunayasikia mitaani kwamba Matumla analalamika wakati yote hayo anayajua tangu mwanzo,” anasema.