Tag Archives: majaliwa

WAZIRI MKUU AWAONYA VIONGOZI WAPYA WA SHIRECU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wapya wa Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga wajipime kama wako tayari kuwatumikia wananchi na kama sivyo waachie ngazi.   Ametoa onyo hilo jana (Ijumaa, Julai 13, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa kijiji cha Mwangongo na vijiji vya jirani mara baada ya kukagua soko la pamba kwenye kijiji hicho, wilayani Kishapu mkoani ...

Read More »

Waziri Mkuu Awasilisha Hoja ya Kuahirishwa Bunge la Bajeti

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa hoja ya kuahirishwa kwa mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti ulioanza Aprili 3 na kumalizika leo Ijumaa Juni 29, 2018. Akiwasilisha hoja hiyo leo bungeni, Majaliwa amesema maswali 530 ya msingi na 1705 ya nyongeza yameulizwa na wabunge. Pamoja na mambo mengine, Majaliwa amezungumzia masuala mbalimbali, zikiwemo halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya ...

Read More »

Waziri Mkuu ‘alinunua’ shule kihalali – Meneja

Na Waandishi Wetu, Lindi na Dodoma   Familia ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ilifuata taratibu zote halali katika kununua Shule ya Sekondari ya Nyangao, iliyopo mkoani Lindi, JAMHURI limefahamishwa. Meneja wa Shule ya Nyangao, Mathias Mkali ameliambia JAMHURI kuwa licha ya taratibu zote kufuatwa aliyenunua shule si Waziri Mkuu Majaliwa, bali aliyenunua ni mkewe Mary Benjamin Mbawala kwa ...

Read More »

WAZIRI MKUU AWAPOKEA WANACHAMA WAPYA 89 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea wanachama saba kutoka vyama vitatu vya upinzani ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) na wengine 82 kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao walikuwa wapiga debe.   Wanachama hao wamepokelewa leo mchana (Ijumaa, Mei 25, 2018) wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua uwanja mpya wa michezo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya ...

Read More »

Waziri Mkuu Aonya wakulima wasiwauzie chomachoma, ataka wasubiri minada

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya wakulima wa ufuta wasikimbilie kuuza zao hilo kwa wanunuzi wasio rasmi maarufu kwa jina la chomachoma bali wasubiri minada itangazwe mwezi ujao.   “Ninawasihi msikubali kuuza kwa akina chomachoma bali tumieni Mfumo wa Stakabadhi za Mazao Ghalani, tumeona mfumo huu ulivyosaidia kwenye korosho,” amesema.   Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Ijumaa, Mei 25, 2018) ...

Read More »

WAZIRI MKUU: SERIKALI INASIMAMIA ELIMU, NIDHAMU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inasimamia kwa karibu miundombinu ya elimu nchini, malezi na nidhamu ili kuhakikisha kunakuwa na usawa katika ngazi zote.   Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Mei 17, 2018) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajab aliyetaka kujua Serikali ...

Read More »

MAJALIWA: SERIKALI IPO MAKINI NA AJIRA ZA WAGENI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Seriali ipo makini na ajira za wageni na itaendelea kuhakikisha kuwa Watanzania wanapewa fursa kwanza.   Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Mei 17, 2018) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Leah Komanya aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ...

Read More »

Tusi gani la kututoa usingizini?

Desemba 6, mwaka jana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitangaza uamuzi wa Serikali wa kuundwa chombo maalumu ili kusimamia eneo la kilometa za mraba 1,500 katika Pori Tengefu la Loliondo. Akasema: “Baada ya kupitia mifumo mbalimbali, timu ya wataalam ilipendekeza kuwa utumike mfumo maalum utakaounda chombo maalum, kwa kuwa una maslahi mapana kwa pande zote husika na unalenga kuleta amani na ...

Read More »

MAJALIWA:TUPO TAYARI KWA FAINALI ZA AFCON 2019

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo tayari kwa maandaalizi  ya fainali za michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.   Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Tanzania. Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei  10, 2018) wakati akijibu swali la Mbungewa Sumve Bw. Richard Ndassa katika ...

Read More »

UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI UMEIMARIKA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa mwaka 2016/2017 na 2017/2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6.   Pia Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuongeza uwezo wa hifadhi ya Taifa ya chakula ...

Read More »

WAZIRI MKUU AIASA JAMII KUMUENZI MZEE MTOPA KWA KUDUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiasa jamii nchini kujiepusha  na migogoro kwa vile haina tija  na badala yake idumishe amani, upendo na uadilifu ili kumuezi mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu  Alhaj Ali Mtopa.   Aliyasema hayo jana (Jumatano, Aprili 11, 2018) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mwanasiasa huyo yaliyofanyika katika kijijini Nanjilinji wilayani Kilwa. Alhaji Mtopa alifariki Jumatatu Aprili ...

Read More »

Waziri Mkuu ataja mafanikio ya JPM

NA MWANDISHI WETU, DODOMA Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametaja mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, na kutoa mwito kwa wananchi kuzidi kuunga mkono juhudi za serikali. Hayo yamo kwenye hotuba yake kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, ...

Read More »

MAJALIWA AKUTANA NA MABLOZI

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchini Urusi na Rwanda kutumia fursa hiyo kwa kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii. Pia amewataka Mabalozi kila mwisho wa mwaka wajifanyie tathmini ya mafanikio waliyoyapata kutokana na uwakilishi wao katika Mataifa ambayo  ni kwa kiasi gani wamechangia kwenye uboreshaji wa maendeleo ...

Read More »

Amlawiti binti, mahakamani majaliwa

DODOMA EDITHA MAJURA Mwanafunzi wa Darasa la Nne, anayesoma shule iliyopo Kata ya Nzuguni, (majina yanahifadhiwa kimaadili) amekuwa akilawitiwa na mwendesha pikipiki, maarufu kama bodaboda tangu mwishoni mwa mwaka jana hadi mwaka huu, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Taarifa hizi zinaibuka ikiwa ni mwezi mmoja tangu JAMHURI liliripoti habari za mwanafunzi mwingine wa shule hiyo, kushindwa kuendelea na masomo ya Darasa ...

Read More »

Waziri Mkuu Asema Serikali Itaimarisha Masoko ya Mazao Nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija. Aliyasema hayo jana (Februari 2, 2018) wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko. Alisema kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko  ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi. “Kupitia Wizara ya Kilimo ...

Read More »

WAZIRI MKUU AKABIDHI KADI ZA MATIBABU KWA WAZEE 280

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amegawa kadi za matibabu kwa wazee 280 wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, kadi hizo zitawawezesha wazee hao kutibiwa bure. Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa matibabu bure kwa wazee walio na umri wa kuanzia miaka 60. Waziri Mkuu alikabidhi kadi hizo jana (Alhamisi, Januari 18, 2018) alipotembelea ...

Read More »

WAZIRI MKUU ASIMAMISHA UUZAJI WA MALI ZA KNCU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bibi Anna Mghwira asitishe uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU). Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime. Hatua hiyo imekuja baada ya KNCU kutangaza kuuza shamba lake kwa ajili ya ...

Read More »

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWATAKA WANAUME WA TARIME WAACHE UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaasa wanaume wa wilaya ya Tarime kujiepusha na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuachana na kilimo cha bangi. Alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime. Waziri Mkuu alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na ...

Read More »

MAJALIWA: SIJARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA SIRARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa kituo cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya. Kufuatia hali hiyo amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  afike ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma akiwa na mkandarasi aliyejenga kituo hicho. “Serikali haiwezi kuvumilia ujenzi wa hovyo kiasi hiki, namtaka Kamishna wa TRA aje ...

Read More »

WAZIRI MKUU ATATUA MGOGORO WA MIAKA MITATU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara ambao umedumu kwa miaka mitatu. Ametoa uamuzi huo leo (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Halmashauri ya Mji wa Tarime. Amesema amesitisha mpango huo wa ujenzi wa makao makuu ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons