Mfumo wa sasa wa ufadhili wa ligi hauna
tija kwa taifa, kwani tunaendelea kuzifadhili
Simba na Yanga ambazo kitaifa hazina
uwezo, wameshuka kisoka ndiyo maana
hawashindi. Turudishe mfumo wa Sunlight
au Taifa Cup kupata wachezaji wazalendo
kutoka vijijini na wilayani.
Msomaji wa JAMHURI, Pangani,
0716612960

Lindi hatuna DC
Kutokuwa na mkuu wa wilaya Lindi Vijijini
kunawanyima uhuru wananchi kuamua
mambo ya maendeleo. Mkoa wa Lindi una
wilaya sita, lakini moja haina mkuu wa
wilaya. Tunaomba Rais wetu, John

Magufuli, aliangalie hili.
Issa Mandalu, Rondo, Lindi, 0785103647

Kuuli umetumwa?
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF
amedai uchaguzi wa Simba una kasoro
nyingi, pia fomu ni gharama. Mbona
inaingilia mamlaka ya kamati yetu? Kamati
yetu ina wasomi zaidi ya wewe.
Umetumwa?
Msomaji wa JAMHURI, 0711558059

Tutangaze utalii
Watanzania tuwe mstari wa mbele
kuutangaza utalii wetu duniani kote. Vitu
vizuri vinapaswa kuwekwa kwenye
mitandao ya kijamii, hivyo wananchi
waruhusiwe kupiga picha maeneo ya utalii
na kuziweka katika mitandao ya kijamii
badala ya kuweka picha chafu na habari za
kipuuzi.
Issa Mandalu, Rondo, Lindi, 0785103647

Bodaboda

Kero yangu ni kwa madereva wa bodaboda,
baadhi yao wamegeuza pikipiki zao kuwa
uwanja wa singeli. Utamwona yupo kwenye
mwendo wa hatari, hana kofia ngumu wala
viatu rasmi na kupiga muziki kwa sauti za
juu kama wako kwenye vigodoro.
Wasimamizi wa vyombo hivi waangalie hilo.
Issa Mandalu, Rondo, Lindi, 0785103647

TARURA
Ninaomba uongozi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo na Tarura mkarabati
barabara ya King’ong’o – Matosa kwani ni
mbaya sana, ina mahandaki makubwa
yaliyojaa maji yanayovuja kutoka kwenye
mabomba ya Dawasco na maji taka
yanayotoka kwenye majumba ya watu.
Kimaro Nkuhungu, Dodoma, 0784581952

Kulikoni ajali hizi?
Wakati umefika Watanzania kujinyenyekeza
mikononi mwa Mungu kutaka ufunuo
kuhusu matukio ya ajali mbalimbali
zinazotokea kila kukicha. Biblia Takatifu

katika Yeremia 33:3 inasema niite, nami
nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo
makubwa, magumu usioyajua.
Msomaji wa JAMHURI, 0682880266

RC Makonda
Kuna uwezekano mkubwa jeuri ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,
inatoka kwa baadhi ya vigogo wanaomtumia
kwa masilahi yao. Hata hayo makontena
huenda si mali yake. Wakati umefika Rais
Magufuli amtumbue kwa manufaa ya
Serikali ya Awamu ya Tano na Ikulu pia.
Msomaji wa JAMHURI, 0682880266

IGP tusaidie
Tunaumizwa na uchotaji mchanga huku
Madale Mto Nakasangwe, polisi Kituo cha
Madale rushwa hupokea kutoka kwa
madereva na kushindwa kuwashughulikia.
IGP tunaomba ufanye mabadiliko katika
Kituo cha Polisi Madale ili tusikilizwe na
kunusuru nyumba zetu.

Msomaji wa JAMHURI, 0655619412

Hongera JAMHURI
Kwanza kabisa nalipongeza Gazeti letu
pendwa la JAMHURI kwa kutusemea sisi
Watanzania ambao tulikuwa hatuna mahali
pa kupazia sauti zetu. Watumishi wa gazeti
hili mnastahili pongezi zetu Watanzania,
tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu azidi
kuwatia nguvu mwendelee kutusemea, tuko
pamoja nanyi.
Binamungu, Mwanza, 0746620152

Mashabiki Simba
Naomba kuwasihi mashabiki wa Timu ya
Simba kuwa kitendo cha kumdhihaki kocha
hakipendezi. Wakumbuke kuwa timu yao
inajipanga kwa mechi za kimataifa hapo
baadaye, na ili kufanikiwa ni lazima kuwe na
maandalizi makubwa ya kiufundi; wawe
wavumilivu, yajayo yatawafurahisha.
Samora John, Karatu, 0717479457

Bima
Nashauri vyombo vyote vya majini

vinavyosafirisha abiria bila kujali ukubwa
wake pamoja na gari la moshi iwepo bima
ya lazima kama ya magari kusudi
inapotokea ajali fidia sitahiki ilipwe na
kampuni ya bima.
Projest Iluganyuma, 0713770738

SUMATRA
Dhamira yangu leo ni kutoa maoni juu ya
utendaji wa Sumatra. Inavyoonekana
mamlaka hiyo imezidi kukaa kimya bila
kuyatolea maelezo matukio ya vyombo vya
usafiri wa baharini. Kuna matukio mengi ya
ajali za majini lakini mamlaka haijachukua
hatua zozote. Je, hawaoni matukio hayo?
Salim Liundi, Mtoni kwa Azizi Ally, Dar es
Salaam, 0763036009

Mikataba mibovu
Ni wakati mwafaka sasa Takukuru
iwakamate watu wote waliosaini mikataba
mibovu nchini na kuwafikisha mahakamani.
Mikataba ya madini, umeme, gesi na mali
asili nyingi za nchi yetu ni mibovu. Wako
baadhi ya viongozi walioishi maisha ya

anasa sana na kuwasababishia
Watanzania umaskini mkubwa kwa
kunufaika na mikataba hiyo.
Msomaji wa JAMHURI, 0753022292

Walipa kodi tunaonewa
Rais John Magufuli akiwa jijini Mwanza
alitoa agizo kuwa wamachinga
wasibughudhiwe hadi hapo watakapopatiwa
maeneo rafiki. Sasa ni mwaka
wa tatu viongozi wa mikoa, manispaa bado
hawajapata maeneo rafiki? Haki iko
wapi? Wanaolipa kodi wazibiwe milango
yao ya maduka na wasiolipia kodi?
Msomaji wa JAMHURI, 0713495168

Waziri wa Sheria
Naomba kumuuliza Waziri wa Sheria na
Katiba wa Tanzania, kwa kuwa serikali
ilishindwa kuridhia sheria za kimataifa
zinazosimamia meli na vivuko nchini, je,
hawa wanaotuhumiwa kuangusha kivuko
cha MV Nyerere watawashtaki kwa sheria
gani?
Mutakyahwa, Mwanza, 0767664927

Makondakta
Kwa nini baadhi ya makondakta wana kauli
chafu kwa abiria? Na hawajali abiria wao,
tunaomba serikali ilitazame suala hili.
Hairat Juma, Singida, 0693476306

Vyama vya upinzani
Tuna miaka 26 ya vyama vingi lakini ni
ajabu kwa vyama vyetu vya upinzani
kutoelewa dira yao ni ipi, badala ya kusubiri
matukio na makosa ya serikali. Tukiambiwa
tutasubiri sana tunapandwa jazba.
Msomaji wa JAMHURI, 0782205796

Wahujumu uchumi
Watu waliojenga nyumba za kulala wageni
ndani ya Hifadhi ya Serengeti ni wahujumu
uchumi wa nchi. Kibaya zaidi ni hao watu
kujenga kwenye njia wanayopita wanyama,
huku ni kuvunja sheria za nchi. Sheria
ichukue mkondo wake, kwani hata wafugaji
hawaruhusiwi kuchunga ndani ya hifadhi.

Msomaji wa JAMHURI, 0753022292

Muhimbili balaa!
Vipimo vya MRI, T-Scan katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili ni ghali sana. Serikali yetu
makini inayojali Watanzania wanyonge
iangalie gharama hizi, pia ianzishe kliniki
maalumu ya kupima magonjwa ya moyo na
kansa zote ikiwemo tezi dume na mengine.
Msomaji wa JAMHURI, 0753022292

Mawasiliano
Huduma za mawasiliano mkoani Iringa, Kijiji
cha Mgongo, Msisina hatuna mawasiliano
ya simu, tunasumbuka sana. Serikali
ituangalie.
Msomaji wa JAMHURI, 0689444027

Brigedia Mbenna mkweli
Nimesoma sms katika Gazeti la JAMHURI
la Septemba 25 hadi Oktoba 1, mwaka huu
iliyoandikwa na mtu ambaye hakutaja jina

ila anaishi Mwanza. Anadai Brigedia
Mbenna anapandikiza chuki katika mfumo
wa vyama vya upinzani kwa kuandika
mambo ya enzi zilizopitwa na wakati za kina
Hitler na Krugger. Nataka kumjulisha ndugu
yangu kuwa yule sisi tunamfahamu kuwa
hana itikadi ya chama chochote cha siasa.
Mwache huyu mzee aendelee kutuelimisha.
Lusian Ngoromera, Morogoro, 0783473547

Mauaji yanatisha Ulanga
Waziri Kangi Lugola tunaomba vituo vya
Polisi Iragua na Mtimbira, wilaya za Malinyi
na Ulanga, maeneo hayo ni mauaji tupu
siku za minada. Tutashukuru sana kama
utasikia kilio chetu.
Lusian Ngoromera, Morogoro, 0783473547

Ajali zinatumaliza
Kila Mtanzania ana huzuni kutokana na ajali
ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea wiki
iliyopita, tunaona kama ni ndoto au
tunaangalia sinema fulani, ila ndio ukweli

wenyewe kwamba ndugu zetu wametutoka,
hatuna cha kufanya zaidi ya kusema Mungu
alitoa, tena ametwaa. Jina lake lihimidiwe.
Majuto, Magazeti, Iringa, 0755940530

Miss Tanzania
Hongera sana Miss Tanzania 2018 kwa
ushindi mnono, ila una deni la kuelimisha
jamii ya Kitanzania na uonyeshe mfano kwa
ma-miss wote waliopita kwamba wewe uko
tofauti na wao.
Majuto, Iringa, 0755940530

OCD Mugumu
Waziri Lugola mwondoe OCD hapa
Mugumu, ni kero mno. Septemba 24,
mwaka huu wamekamatwa wezi wa
ng’ombe zizini katika Kijiji cha Masinki,
Kitongoji cha Magange na kuuawa na
wananchi wenye hasira. OCD aliamuru
askari wake kuwakamata vijana kitongoji
kizima na kuwataka watoe Sh 50,000 ili
waachiwe. Huu ni uonevu.

Msomaji wa JAMHURI, 0759030344

Askari waache ubabe
Askari wetu kama askari wa makaburu wa
Afrika Kusini. Suala la usafi ni muhimu
sana, lakini hawa jamaa wanaondoa dhana
ya polisi. Badala ya kutoa elimu wanatumia
nguvu nyingi kuliko jambo lenyewe. Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda, unafanya kazi vizuri lakini hawa
wanakuharibia.
Msomaji wa JAMHURI, Dar es Salaam,
0716988670

Hongera TFF
Nalipongeza Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kwa kutoa tamko kuhusu mashabiki
kwenda Cape Verde. Kwa kweli mmefanya
vizuri, endeleeni hivyo hivyo, taifa mbele.
Frank Mwihava, Iringa, 0769965618

NEC haina aibu?

Haiingii akilini kukubaliana na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) kudai wapinzani
ndio hukumbwa na dosari za kutojaza fomu
za uchaguzi ipasavyo pamoja na mawakala
wa vyama vya upinzani. Ni kweli CCM iko
makini? NEC acheni ubabaishaji.
Msomaji wa JAMHURI, Arusha,
0787683360

CWT mko wapi?
Mimi ni mdau mkubwa wa elimu hapa
nchini, lakini nashangazwa na idadi kubwa
ya walimu kuishi katika nyumba
zilizoezekwa kwa makuti vijijini wakati hapa
jijini wana hisa yao ya jengo la Mwalimu
House. Wanafanya kazi katika mazingira
magumu sana.
Salim Liundi, Dar es Salaam, 0763036009

Mwisho …………..

754 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!