Wapendwa wasomaji wetu salaam,

Kwa muda wa mwezi mmoja sasa tangu Januari 29, 2015 mtandao wetu haukuwa hewani kutokana na ujambazi wa mtandaoni (hacking). Hatujui ni nani, ila mtandao wetu ulitekwa na ikawa hatuwezi kuingia kuweka habari au vinginevyo. Kwa sasa naomba kumshukuru kipekee Maxence Melo kwa utaalam wa hali ya juu ameweza kubaini ujambazi huo na kuturejesha mtandaoni.

Kuanzia sasa tutaongeza usalama wa mtandao wetu na kudhibiti ujambazi huu kuhakikisha tunaendelea kuwapa habari ngumu (hard news) bila woga wala wasiwasi.

Nawashukuru kwa kutuvumilia na kwa kuwa tumerejea, tutalazimika kuweka matoleo yote kwa mpigo ambayo hatukuweza kuyaweka mtandaoni kutokana na tatizo nililolitaja hapo juu.

Tunawashuru kwa kuendelea kutuunga mkono na kulifanya Gazeti la JAMHURI kuendelea kuongoza katika soko la magazeti hapa nchini.

Asanteni sana,

Deodatus Balile

Mhariri Mtendaji,
Jamhuri Media Limited

1389 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!