Tunza sura yako ivutie

Kila mtu anapenda sura yake iwe laini, nyororo ya kung’aa. Wakati mwingine sura zetu huchakaa kutokana na mihangaiko ya hapa na pale. Zifuatazo ni hatua za awali za kutunza ngozi ya sura yako ionekane vizuri.

Ukijua aina ya ngozi yako itakusaidia kujua ni bidhaa gani utumie katika ngozi yako. Kuna ngozi zenye mafuta, kavu, za kawaida na nyepesi kuonesha mabadiliko.

 

Usafi wa mara kwa mara utakuondolea vumbi, vipele vidogo vidogo na uchafu ulioganda katika ngozi. Tumia kitambaa safi na safisha uso wako mara mbili kwa siku.

Fuata ratiba ya usafi wa ngozi yako ya uso katika muda ule uliojipangia kila siku.

 

Ushauri wa wataalam ni muhimu kabla ya kutumia bidhaa yoyote. Itakusaidia kuepuka madhara ya ngozi.

 

Tumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake kwenye kampuni zinazotambulika. Ukipenda bidhaa za bei rahisi kuepuka gharama tumia bidhaa asilia.

 

Zingatia aina ya vyakula kwani kutumia bidhaa sahihi katika ngozi yako pekee yake haitoshi. Chakula pia kinaathiri mwonekano wa ngozi ya uso wako. Epuka vyakula vyenye mafuta, mchanganyiko wa matunda na mboga kupita kiasi. Kunywa maji mara kwa mara.