Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema), ameshangazwa na kilio kikubwa cha twiga bungeni ikilinganishwa na thamani ya watoto 360,000. Ifatayo ni kauli ya mbunge huyu neno kwa neno. Endelea…

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana kwenye hili Bunge wabunge tulifanya kitu kinaitwa Mob Justice tulipokuwa tunashughulikia suala la Mheshimiwa Ezekiel Maige kwa sababu tu Wizara yake (Wizara ya Maliasili na Utalii) ilionekana kwamba wamepoteza twiga wawili.

 

Sasa naomba nianze kwa kusema kwamba duniani hapa tunaangalia opportunity cost (gharama ya fursa), thamani ya twiga wawili ukipeleka kwenye soko, lakini wanafunzi 360,000 wa Tanzania waliopata ziro thamani yao ni kubwa kuliko twiga wawili waliopotea.

 

Lakini leo watu wanashangaa kwa nini hotuba ya Mkuu wa Kambi ya Upinzani inataka Mheshimiwa Waziri Shukuru Kawambwa ajiuzulu. Kama tulimwadabisha Mheshimiwa Maige kwa sababu ya twiga wawili, tukamwajibisha Mheshimiwa Chami kwa sababu ya TBS sijui magari yamepimwa hovyo hovyo huko nje ambapo thamani yake ukikadiria haivuki shilingi milioni 200.

 

Lakini leo tunakataa tena ninyi mnaunga mkono kwamba mnashangaa kwamba kwa nini Mheshimiwa Mbowe kwenye speech yake anataka Mheshimiwa Shukuru Kawambwa ajiuzulu! Yaani hao twiga kweli wawili wana thamani kuliko watoto wa Tanzania 360,000 ambao wamefeli na hatma yao mpaka sasa haijulikani na ndiyo maana [nasema] this is pathetic!

 

Yaani kuna Mzee mmoja anaitwa Mheshimiwa Chiligati (John Chiligati) hawa ndiyo waliowahi kuwa mawaziri, alipokuwa anazungumza hapa alisema kwamba yeye analinganisha ubora wa elimu- yaani kwake ubora wa elimu ni wingi wa madarasa bila kuangalia output inayotoka kwenye hayo madarasa na Baraza la Mawaziri ndiyo think tank, hii ndiyo injini inayoendesha hii nchi! Sasa kama nchi ilikuwa inaendeshwa na watu kama hawa ndiyo maana leo tupo kwenye hii mess tuliyonayo leo.

 

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nikuambie kwamba hali ya elimu kwenye nchi hii ni pathetic, watoto wanakaa chini kwenye shule zote ndani ya miaka 50 ya Uhuru kwenye nchi ambayo imejaa misitu ambayo inatoa mbao mpaka mbao nyingine mnasafirisha kupeleka nje, lakini watoto wanakaa chini!

 

Ndiyo maana tunazungumza, na ninyi ndiyo mnatupa hoja za kuzungumza kwa sababu mmefumbia macho matatizo ya msingi ya Watanzania, ndiyo maana tunasema leo kwa mfano nauli za daladala zimepanda kwa sababu gharama ya kuendesha shughuli ya daladala iko juu kwa sababu vipuri vyote vya magari wana import kutoka nje, pesa ya Watanzania thamani yake inashuka against dola kwa hiyo unaposafirisha vipuri yaani unapoingiza ni lazima bei iende juu kwa hiyo gharama ya kuendesha shughuli za daladala zinapanda kwa sababu pesa imeshuka thamani, hii haihitaji magic.

 

Halafu Mheshimiwa rafiki yangu Bwana Lusinde anasema namna ya kupeleka thamani ya … sasa kwa hiyo yaani ninyi mmeruhusu nchi hii ndiyo maana rafiki yangu Mheshimiwa Msigwa anasema yaani ninyi mmeruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa kwenye nchi hii na ndiyo maana tupo hapa. Sasa kama mko hapa mnapigianapigiana makofi wakati hii nchi ipo kwenye mess this is pathetic!

 

Ndiyo maana nadiriki kusema kwamba hii mmetuweka katika state ambayo this Government I can really say, I can dare say and I want to go into history that I have said the Government is impotent, it is incompetent and it is governed by lords for poverty…people!

 

Naomba niseme hivi, kwenye haya mabaraza ya Katiba, ukisoma hiyo hotuba ya Mheshimiwa Mbowe imejaa solutions nyingi tu, nyingi tu zimejaa kwa sababu ya narrow interpretation ya watu wengine wanasema eti hii tunalalamika. Tumeshawashauri mara nyingi mpaka tumechoka, kama hamsikii mmeshauriwa kwa miaka 50 bado nchi inapiga hapo mark time, sasa tuwafanyaje? Yaani ninyi mnataka tuje hapa tuwapongeze kwa kuumiza nchi!

………………………….

 

Naibu Spika na lugha za matusi bungeni

Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema) aliomba mwongozo wa Spika kutokana na maneno aliyoyaita ya kuudhi kutoka kwa Mbunge wa Konde, Muhamed Seif Khatib (CCM).

 

“Mwongozo ninaouomba, rafiki yangu Mheshimiwa Khatib Mbunge wa Konde alivyokuwa anazungumza amediriki kutumia lugha ambazo hazistahili kutumika hapa Bungeni kwa kusema akasema na mlisikia wote kwamba Mheshimiwa Mbowe alikuja hapa akajamba halafu akaenda. Sasa naomba nimalizie kwa kusema inasikitisha sana kama hawa watu wenye umri kama huu wanafurahia maneno ya kitoto kama haya. Nashukuru.”

 

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kelele zote humu ndani zinaonyesha jinsi ambavyo sasa mnazifahamu Kanuni na mnaona kabisa pale mahali ambapo Kanuni zinakuwa hazizingatiwi na moja ya maeneo ambayo mara nyingi sana tumesimama na kusisitiza ni eneo hili la kuwa na lugha ya staha ndani ya Bunge. Kwa manano mafupi tunasema lugha ya kibunge. Yapo maneno hutarajiwi Mheshimiwa Mbunge kuyatamka.

 

Sasa hii ni Wizara ya kwanza katika mlolongo ambao ninyi mnafahamu katika zoezi zima ambalo tunaendelea nalo la Bajeti litakalochukua hadi mwezi wa sita mwisho. Sasa kwa Wizara ya kwanza tukianza kwa lugha hizi mimi sina hakika kama tutafika mwisho. Wako Waheshimiwa Wabunge ambao wamechangia hoja ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, wamezungumzia matatizo ya wananchi, wamefikisha hoja kwa heshima, kwa ustaarabu na hao nawapongeza sana .

 

Sasa wako wengine ambao walisamama wao lengo lao lilikuwa ni kukashifu na kutukana na kutumia maneno yoyote yale ya kuudhi sijui kwa madhumuni gani. Sasa niseme tu kwamba hizi kesi ukizitazama ziko nyingi zinazojirudia. Mimi kwa hatua hii nitoe karipio kwa wote ambao wamekuwa wanajihusisha na lugha ambazo hazikubaliki humu bungeni na niwaambie wananchi wanaotusikiliza hawafurahishwi hata kidogo na hiki kinachoendelea.

 

Nafikiri hata wale waliokuwa wanatetea Bunge liwe live sasa wanatuelewa kwanini baadhi walikuwa wakifikiri kwamba iko haja ya kuwa na aina fulani ya mchujo ili kuondokana na baadhi ya vitu ambavyo vinaenda ambavyo havikupaswa kuwepo hata mara moja. Sisemi kwamba hilo ndilo lengo la Bunge, ‘hapana.’

 

Lakini niseme kwa kweli tunawaomba sana Waheshimiwa wabunge, mmesikia wabunge wanaowakilisha matatizo ya wananchi wanazungumza vipi, tuwaige hao. Hatujaja hapa kutukanana, hatujaja hapa kuvunjiana heshima. Dakika zenyewe tano au kumi; wasilisha matatizo ya wananchi.

 

Kwa hiyo huo ndiyo mwongozo wangu kwa wote kabisa waliohusika na waliotajwa, sina haja ya kurudia jina moja moja, tujichunge kuanzia sasa tuendelee kufanya kazi yetu ya kibunge kama wabunge na meza hii haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kuanzia sasa kwa wale ambao wataendelea na tabia ya kutumia maneno ambayo kwa kweli hayakubaliki katika jamii ya Kitanzania hivihivi kirejareja.

 

 

1019 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!