Ningependa nioneshe pia kuwa wapo wasomi wasiojiamini kabisa ingawa wana shahada za vyuo viikuu. Kama si upotoshaji wa kukusudia, basi hawana elimu (not liberated mentally), ni wajinga ingawa wamesoma (have been to school but not educated).

Nitoe mifano michache. Yupo msomi wa Chuo Kikuu kaandika vitabu kadhaa na matoleo kadhaa, lakini amenishangaza kwa upotoshaji wake wa makusudi kabisa katika kitabu chake (prejudicial writing).

Mathalani, kitabu kile “The Untold Story of the Muslim Struggle against British colonialism in Tanganyika” kimeandikwa na ndugu Mohamed Said na kuchapwa Minerva Press LONDON, ATLANT, MONTREUX SYDNEY. Nimeshangazwa kuona vitu kama, namnukuu; “in the legislative council Africans were represented by a CATHOLIC PRIEST, Fr. Gibbons who did not even live among Africans but at Minaki Mission outside Dar es Salaam” (uk. 42 kitabu chake hicho).

 

Huyu mwandishi kama sikosei naamini alisoma shule ya Wakatoliki iliyokuwa ikiitwa St. Joseph’s Convent School (Forodhani) tangu elimu ya msingi hadi sekondari.

 

Alisoma kidato cha kwanza hadi cha nne miaka ya 1967-1970. Kila Ijumaa wakati wa swala ya Ijumaa aliruhusiwa kwenda msikitini na baada ya swala zile walikuwa “off”. Bwana Mohamed Said na Mwislamu mwenzake aliyeitwa Said, walipewa fursa ya kupata kipindi cha dini yao na walifundishwa na sheikh mmoja aliyeitwa Mohamed. Analielezaje hilo la fursa namna hii shule za Waislamu zingeruhusu afanye hivyo?


Mohamed Said ni mtoto wa mjini Dar es Salaam, kazaliwa maeneo ya Gerezani. Cha ajabu kwangu ni kuona kwanini hakunukia Ukatoliki maadamu kasomåea shule ya Wakatoliki? Alikoseaje hadi ampakazie Mwalimu Julius Nyerere kwa maneno yake yale, ninayanukuu; “…Had been through a system which moulded its followers to be loyal to both the Church and the State…” (uk. 112 wa kitabu chake kile).


Basi, ingekuwa rahisi hivyo huyu ndugu angekwisha kuwa “moulded” katika Ukatoliki. Mbona amebaki Mwislamu safi na Mswalihina safi? Ndiyo kithibitisho kamili kuwa shule za Wakatoliki zinatoa “secular education” kama aliyopata huyu ndugu, kamwe haziwapakazii watoto Ukristo kama vile Uislamu unavyosilimisha wote wanaosoma katika shule zao. Elimu dunia ni haki ya kila mtoto – haina dini kabisa.

 

KWELI HAJUI KUWA MINAKI NI MADHEHEBU YA UMCA – Anglicana? Hajui kweli kuwa Padre Mkatoliki hawezi kukaa Minaki? Iweje kuingiza neno KATOLIKI kwa namna hii? Sasa kwa taarifa sahihi, Canon Gibbons aliyekuwa Kasisi wa Anglikana na Mwalimu wa St. Andrews Minaki ni Mwingereza “pyua”. Hapo Ukatoliki unaingiaje katika fikra za mwandishi? Kwa vile yeye (mwandishi) ni Mwislamu na ameambiwa kuwa kuna Ukatoliki hapa na kwa kuwa anauchukia, basi kivuli kile cha Ukatoliki kimempagawisha hadi akaandika uongo.

 

Si kosa hilo tu, lakini bado anauchukia Ukatoliki kiasi kwamba katika kitabu chake hicho hicho amewanakili wengi kimakosa. Katika uk. Wa 112 katika kitabu hicho hicho ameandika haya na nukuu, “Nyerere was a Roman Catholic Trained teacher who had been through a system which moulded its followers to be obedient and loyal to both church and the state”.

 

Hapa ndipo anajionesha umbumbumbu wake kihistoria. Nyerere kasoma shule ya msingi ya Serikali Mwisenge (si misheni), akaja Tabora Government School (si misheni), kaenda Makerere University College (si misheni) – hakupitia hata shule moja ya misheni, angewezaje kukuzwa Kikristo wakati hata hiyo dini ya Ukristo kaingia mwaka 1943 akiwa mtu mzima? Ni kivuli cha Ukatoliki kilimsukuma aandike upuuzi namna hii – rejea historia ya Mwalimu by H. A. K. Mwenegoha printed by General Printers Ltd. Homa Bay Road S.L.P 18003 Nairobi Kenya uk. 2 na 4-5) utaona historia ya Nyerere. Hakuna palipoandikwa kasoma shule ya Wakatoliki. Hangeweza kamwe kuwa Roman Catholic trained teacher! Mbona mwandishi kasoma shule ya Wakatoliki na hakuwa “moulded” kikatoliki?

 

Katika uk. 130 wa kitabu hiki cha Bwana Mohamed Said anatoa kosa la mwaka hata haliweza kusameheka kwa Wakristo wala Waislamu wenzake. Ameandika hivi, namnukuu tena; “The only person who is known to have complied with that condition was Mwalimu HARUBU SAID of St. Mary’ School Tabora”. Mama yangu we! Kwa Wazungu wangelia kwa kosa namna hili wangetumia neno “atrocious”.

 

Wakati wa ukoloni shule ziligawanyika kidini. St. Mary’s ni ya Wakatoliki tu sasa isingeliwezekana Mwalimu Mwislamu wa pale Tabora akafundisha shule ile! Huyu Mwalimu Harubu Saidi alimaliza Makerere mwaka 1938 na akaanza kufundisha Tabora Government Boy’s School shule ya Serikali mwaka 1939 na ndiye aliyemfundisha Nyerere Std VII-X hadi mwaka 1942 alipohitimu Tabora na kwenda Makerere.


Hili ni kosa lisilosameheka kwa Mwislamu kufundisha shule ya Katoliki enzi zile za ukoloni. Sasa ndugu yangu Mohamed Said amewapotosha wengi kweli kwa kitabu chake kilichochapwa Ulaya na ninaamini kwa msaada wa wafadhili wa kigeni kwani hakuwa na mtaji wa kukichapisha nje.

 

Hapo ni wazi kivuli cha Ukatoliki kilimtisha sana hata akaomba msaada kichapishwe nje kuonesha Waislamu walivyokandamizwa na Ukristo! Wasomi mnakubali uongo na upotoshwaji wa aina hii? Je, Uislamu ndiyo chuki ya namna hiyo isiyo na kichwa wala miguu ya kusimamia?

Ningeweza kuendelea kuonesha makosa namna hiyo katika kitabu hicho mengine yapo kwenye uk. 217 juu ya Mwalimu George Magembe.


Katika uk. 206 juu ya Wamakonde wa Mtwara, Bwana Said anathubutu kuuhakikishia umma kwa kusema, namnukuu tena; “The Makonde of Tanganyika residing in Lindi, Mikindani and Mtwara along the Southern Coastal belt are predominanthly Muslims. Non-Muslim Makonde could be noticed by the marks in their faces and the piece of wood inserted into the lower lip of the mouth of their women”.


Sijui mwanamke wa Kimakonde hata mmoja aliyetoboa NDONYA (yeye anaita a piece of wood) katika mdomo wake wa chini. Hii inaoneshwa wazi hajawaona akina mama wa Kimakonde wenye ndonya wala hiyo ndonya haijui, wala hajaiona, bali amesikia kwa aliyemwelezea akakurupuka kuandika kitabu chake hiki. Na Wazungu waliopitia kitabu hiki wakaamini hilo. Waulizeni Wamakonde juu ya ndonya. Ni mila ya akina mama wa zamani wa Kimakua, Kimwera na Kimakonde (sisi tukiwaita Wamawia).

 

Kwa mifano hii mnaweza kuona jinsi wasomi Waislamu wanavyouchukia Ukristo hasa Ukatoliki na kuupakazia kama vile mbwamwitu alivyomdhamiria yule mwanakondoo mradi ipatikane sababu ya kuuponda Ukristo, basi Mwislamu atauponda tu. Hii ni tabia ya MFUMO ISLAM.

 

Kitabu hiki cha msomi Bwana Mohamed Said kimetolewa kwa heshima (dedicated to) ya Profesa Kighoma Ali Malima. Kwa bahati nzuri sana huyu Profesa mimi namjua vizuri tangu ujana wake tukiwa katika TYL (Umoja wa Vijana wa TANU) na alipokuwa Katibu wa Vijana Wilaya ya Tunduru mwaka 1960 tulishirikiana kwenye Uchaguzi wa Mseto wa Mbunge wa Tunduru. Hakuwahi hata mara moja kuonesha chuki kwa Ukristo hasa Ukatoliki. Tukiwa hapa Dar es Salaam mara nyingi nimemkaribisha kuzungumza na Vijana wa JKT Mgulani masuala ya uchumi.

 

Nchi zote zenye “MFUMO ISLAM” zimeiga tabia ya Kiarabu ya kuhamaki na kupenda shari ilimradi wapigane. Angalieni Iran, Iraq, Misri, Libya, Morocco, Algeria, Pakistan, Afghanistan kila siku Waarabu watazua jambo ili wauane. Mbona Indonesia kuna Waislamu wengi kuliko taifa lolote ulimwenguni hawauani? Imani ya Kiislamu ni upendo, kuvumilia, kuswali, kutoa zaka na kusaidia masikini ambao ni wahitaji.

 

Leo hii sisi ndugu wa Taifa la amani tunapakaziwa na wageni wa kuja nchini kwa kisingizio cha imani ya dini. Indonesia hawana imani namna hiyo? Uchina hawapo Waislamu? Malaysia hawapo Waislamu? Kwa nini madai ya dini yaletwe barani Afrika tu na hasa Mali, Nigeria na sasa huku Afrika Mashariki?

 

Mimi nawasihi ndugu zangu Waislamu uhalali wa imani yao si kisingizio cha kuwalazimisha wengine wawe kama wao. Upo usemi wa Kiingereza unaosema hivi, “Someone’s honey is another’s poison?” Kitamu kwako ni kichungu kwa mwenzio.

Brigedia Jenerali mstaafu Francis Mbenna anapatikana katika simu 0715 806758. Alikuwa mwalimu wa sekondari na Afisa wa JWTZ. Ni mwanahistoria na ameandika kitabu cha HISTORIA YA ELIMU TANZANIA toka 1892 hadi sasa (Dar es Salaam University Bookshop).


1184 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!