Nyerere: Elimu inayotolewa ituwezeshe kujiamini

“Elimu inayotolewa lazima ijenge akili ya kuuliza, uwezo wa kujifunza na uwezo wa kujiamini kama raia huru na sawa katika jamii.”

Maneno haya ni ya Mwasisi na Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Thatcher: Mwanaume husema, mwanamke hutenda

“Kama unataka kilichosemwa, uliza mwanaume; kama unataka kilichofanyika, uliza mwanamke.”

Hii ni kauli ya Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza, Margaret Thatcher.

 

Mbowe: Tusiwachukie wasio wana Chadema

“Wasio wana Chadema si adui zetu. Tuna jukumu la kuwashawishi, kuwabadili wawe wana Chadema, tuongeze idadi.”

Maneno haya ni ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe.

 

Irwin: Propaganda katika uhifadhi wanyamapori

“Naamini matumizi endelevu ni propaganda kubwa katika uhifadhi wa wanyamapori kwa sasa.”

Haya ni maneno ya mtaalamu wa uhifadhi wa wanyamapori wa nchini Australia, Steve Irwin anayejulikana zaidi kama Mwindaji wa Mamba.

Please follow and like us:
Pin Share