Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza amesema kuwa taifa lake linatarajia majibu ya msingi kutokana na kupotea kwa mwandishi wa Saudia Jamal Khashoggi ambaye mara ya mwisho alikuwa katika ubalozi wa Saudi nchini Uturuk

Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Waziri wa mambo ya nje wa Saudia Adel al-Jubeir,Jeremy Hunt amesisitiza kuwa urafiki unapaswa kuzingatia uzingatiaji wa haki muhimu za kibinadamu.

Amesema kama ripoti za vyombo vya habari kuhusiana na jambo hilo vitabainika kwamba ni kweli,basi Uingereza itachukua hatua kali kuhusiana na jambo hilo.

Uturuki inasema kuwa itafanya ukaguzi tu katika eneo hilo la ubalozi wa Saudia ndani ya nchi yake.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudia akizungumzia jambo hilo amesema kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano,na ukaguzi wa wa majengo hayo uendelee kama sehemu ya uchunguzi.

Hata hivyo Saudia imeendelea kushikilia msimamo wake kwamba mwandishi huyo aliondoka katika eneo la ubalozi baada ya shughuli zake,huku Uturuki ikiomba ushahidi kama kweli mwandishi huyo alitoka katika eneo hilo.

Jamal Khashoogi kwa muda mrefu amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa mwana Mfalme Mohammed bin Salman na Jamal alikuwa akiishi uhamishoni nchini Marekani ambapo amekuwa akiandika maoni yake katika gazeti la Washington Post.

By Jamhuri