Balozi wa marekani kwenye Umoja wa mataifa Nikki Haley ametangaza kujiuzulu.

“Imekuwa ni heshima ya maisha” alisema Nikki Hailey akiwa na Rais Donald Trump huko White house alipotangaza kujiuzulu nafasi yake huku akiongeza kwamba haondoki mpaka mwisho wa mwaka.

“Tutakukumbuka sana Trump alimwambia Hailey “umefanya kazi nzuri sana”.
Akimshukuru Haley kwa kazi yake, Trump alimwelezea mwanadiplomasia huyo kama mtu muhimu sana kwake na mtu ambaye ameshirikiana naye na kutatua matatizo mengi akitoa mifano kama ya Iran na Korea Kaskazini.

“Ni matumaini yangu kwamba utarudi tena katika utawala wakati fulani” aliongeza rais Trump akisema unaweza kuchagua kazi nyingine yeyote katika utawala.

“Sina chochote nilichojiandaa kufanya kwa sasa” alisema Haley.

Please follow and like us:
Pin Share