Chama cha Chadema ambacho ni chama kikuu cha Upinzani hapa Tanzania umesema kuwa utawasilisha bajeti yake mbadala bungeni siku ya Jumatatu, waziri kivuli wa fedha na mipango Halima Mdee amesema.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa upunzani kuwasilisha maoni yake tangu mkutano wa bajeti bungeni kuanza miezi miwili iliopita.

Siku ya Alhamisi waziri wa fedha na mipango Dkt. Phillip Mpango aliwasilisha bajeti iliogharimu trilioni 32.5 za Tanzania kwa kipindi cha fedha cha 2018/19.

Kulingana na gazeti la mwananchi , mnamo mwezi Aprili, 2018 kambi ya upinzani iliazimia kutowasilisha hotuba za bajeti na nyingine za upinzani hadi watumishi wa sekretarieti yao ambao mikataba yao hutolewa na Bunge watakaporejeshwa kazini.

By Jamhuri