Serikali ya Guatemala imesema kuwa majivu ya volkano kutoka mlima mmoja unaoendelea kulipuka, yamesababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine ishirini.

Shirika la kukabiliana na majanga nchini Guatemala limesema kuwa mlima Fuego ulilipuka siku ya jumapili, huku majivu hayo yakirushwa hadi kijiji cha El Rodeo na kusababisha uharibifu mkubwa wa makaazi ya watu.

Baadhi yao waliteketea ndani ya nyumba hizo.

Rais wa taifa hilo Jimmy Morales amesema vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhali imetolewa.

Hata hivyo ya watu hao waliokufa kati yao watatu ni watoto.

Mlipuko wa Volcano hii unatajwa kuwa Zaidi tangu ule uliotokea mwaka 1974.

Serikali ya Guatemala inasema kuwa takribani watu milioni moja wameathirika kutokana na Volcano hiyo.

Hata hivyo ushauri umetolewa kwa raia kuvaa vifaa vya kuzuia pua zao kutokana na moshi na majivu yanayoendelea kurushwa kutokana na Volcano hiyo.

Watoto kadhaa ni miongoni mwa waliothibitishwa kufariki.

Video zilizochapishwa na vyombo vya habari nchini zinaonyesha miili ikiwa imetapakaa juu ya lava na maafisa wa uokozi wakiwahuhudmia watu waliofunikwa kwa jivu.

Mwanamke mmoja ameeleza kwamba lava ilimwagika katika mashamba ya mahindi na andhani kwamba huedna watu zaidi wamefariki.

Jumla ya watu milioni 1.7 wameathirika na mlipuko huo wa volkano, serikali ya Guatemala inasema.

 

937 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!