Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amefuta mashindano yoyote ya soka yaliyo nje ya mfumo wa shirikisho hilo isipokuwa tu kwa kibali maalum.

Karia ameyasema hayo katika Mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari ambapo amesema mashindano ya soka yasiyo rasmi kama ambayo huandaliwa na wanasiasa majimboni na hata na baadhi ya taasisi na wadau, yamekuwa yakipewa umuhimu mkubwa kuliko mashindano rasmi ya TFF zikiwemo ligi.

“Wakati umefika sasa Wabunge na wanasiasa kwa ujumla watoe fedha kuzidhamini timu za majimboni mwao badala ya kuanzisha mashindano ya ng’ombe na mbuzi”, amesema Karia.

Pamoja na hilo lakini Rais Karia amesaini mkataba wa udhamini wa jezi za timu zote za taifa zikiwemo za vijana na wakubwa kwa wanawake na wanaume. Mkataba huo unathamani ya zaidi ya Sh. Milioni 800.

1262 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!