Watanzania wanaoshiriki shindano la Big Brother Afrika (BBA) wanasaka kwa udi na uvumba kura za kuwawezesha kuendelea katika shindano hilo linalofanyika Johannesburg, Afrika Kusini.

Washiriki pekee kutoka Tanzania wanaowania tuzo ya dola 300,000 za Kimarekani katika shindano hilo ni Feza (25) na Nando (22).

 

Big Brother the Chase linatajwa kuwa ndio jina la shindano hilo kwa mwaka huu, ambapo lilianza rasmi Mei 26, mwaka huu.

Jumla ya washiriki wa shindano hilo ni 28 kutoka nchi 14 za Afrika, yaani Zambia, Uganda,

 

Ghana, Sierra Leone, Nigeria, Botswana, Namibia, Malawi, Angola, Zimbabwe, South Africa, Ethiopia, Tanzania na Kenya.

 

Miongoni mwa washiri hao, Beverly kutoka Nigeria na Huddah wa Kenya wanatajwa kuwa ndio washiriki pekee wenye umri mdogo, yaani miaka 21, huku Angelo wa South Afrika akitajwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa, yaani miaka 36.

Tayari washiriki Huddah wa Kenya na Denzel wa Uganda wametolewa kwenye shindano hilo baada ya kupigiwa kura nyingi za kutoka, huku wenzao Selly wa Ghana, Natasha wa Malawi na Betty wa Ethiopia wakinusurika kwa kupigiwa kura ya kubaki shindanoni.


884 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!