Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema mavuno ya gesi asilia iliyopo mkoani Mtwara yataanza kupatikana baada ya kipindi kisichopungua miaka kumu.

“Kipindi cha kutafuta gesi asilia hadi kuipata si chini ya miaka kumi,” amesema Pinda jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.

 

Pinda alikuwa akizungumza katika hafla ya mapokezi ya vifaa vya kwanza vya ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Hafla hiyo imeratibiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TDPC).

 

Amesisitiza kuwa dhumuni kuu la mradi huo ni kuongeza upatikanaji wa gesi asilia itakayokidhi mahitaji ya matumizi ya nishati ya umeme nchini.

 

“Lengo la mradi huu ni kuinua uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya Watanzania,” ameongeza Waziri Mkuu huyo.

 

Kiongozi huyo ametumia nafasi hiyo pia kutoa wito kwa vyombo vya habari, wanasiasa na wanaharakati kushirikiana na serikali kuelimisha wananchi manufaa ya mradi huo badala ya kupotosha ukweli.

 

Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unajengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na China, na utagharimu Dola za Marekani bilioni 1.225.

 

 

 

 

935 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!