Vijana wengi wa kizazi kipya cha muziki wa Kongo waliowahi kupitia kwa Werrason ni Ferre Gola, Heritier Watanabe, Fabregas, Robinho Mundibu, Bill Clinton, Celeo Scram, Brigade, Capuccino le Beau Gars, Didier Lacoste na Flamme Kapaya.

Tangu mwaka 2000, Werrason anamiliki Shirika lenye majina ya Werrason Fondation, ambalo hutoa misaada zaidi kwa watoto yatima 400.

Kupitia misaada hiyo Werrason ametokea kupendwa na vijana wa mitaani jijini Kinshasa, wajulikanao kwa jina la Bashegue.

 

Shirika lake hilo hutoa misaada pia kwa wanawake wajane, waathirika wa vita, hospitalini pia hupita kuwajulia hali wagonjwa.

Hali hiyo imesaidia kupendwa na Umoja wa Mataifa kwa kupewa tuzo ya Balozi wa Amani.

 Mara baada ya Wenge Musica BCBG kugawanyika na yeye kuunda kundi la Wenge Musica Maison Mere, Werrason aliweza kufanya shoo tatu kabambe jijini Kinshasa mwaka 2015, kwa mara ya kwanza baada ya mgawanyiko huo.

Katika shoo hiyo Werrason alimualika ndugu yake na rafiki yake mkubwa, JB Mpiana.

 

Adiha, aliwaalika pia wanamuziki wakubwa, Papa Wemba na Rogaroga.

Ngiama Werrason alikuwa akifanya matangazo ya kibiashara kutokana na kutolewa kwa albamu yake ya ‘Fleche Ingeta’.

Sifa nyingine ya mwanamuziki huyo ni kwamba aliweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye albamu zote za Wenge Musica 4×4 B.C.B.G Tout-Terrain.

 

Baadhi ya albamu hizo ni pamoja na ‘Bouger Bouger’ ya mwaka 1988, ‘Kin e Bouge’ ya mwaka 1999, ‘Kala yi Boing’ na ‘Le Monde est Méchant’ (single) ya mwaka 1993. ‘Les Anges Adorables volume 1’ na ‘Les anges adorables volume 2’ za mwaka 1994, ‘Pile ou Face’ (solo album ya alain Prince Makaba) ya mwaka 1995, ‘Les Pleins Feux’ yenye nyimbo za marudio ya nyimbo zilizorekodiwa mwaka 1992.

Mwaka 1996 waliachia albamu ya ‘Pentagone’, mwaka 1997 wakatoka na ‘Feux de L’amour’ (solo album ya JB Mpiana).

Werrason akiwa na kundi lake la Wenge Musica Maison Mere, ameshatoa zaidi ya albamu 10 zikiwemo solo albums tatu.

 

Nyingine ni ‘Force d’intervention Rapide’  ya mwaka 1998, ‘Fini la Récréation’ (akishirikiana na ndugu yake Ladins Montana) na ‘Solola Bien’ ya mwaka 1999, ‘Terrain eza Mine’, ‘Kibuisa Mpimpa’, ‘A la Queue Leu Leu’, ‘Tindika Lokito’, ‘Alerte Générale’, ‘Dis l’heure 2 Zouk’ (nyimbo 2) na ‘Témoignage’. 

Werrason aliendelea kufyatua albamum zingine za ‘Sous- Sol’, ‘Temps Présent’, ‘Mayi ya sika’, ‘Techno Malewa sans cesse’, ‘Diata Bawu’,  ‘Techno Malewa sans cesse Suite & Fin’, ‘Satelite+2’, ‘I found a way’ (single),  ‘Education’, ‘Block Cadenas’ (single),  ‘Flèche Ingeta’ na ‘Sans Poteau’ yenye nyimbo zilizorekodiwa mwaka 2007.

Nyimbo mpya za Werrason ni ‘Le Baron des Barions’, ‘Ali Maymona’, ‘Kata Fumbwa’, ‘Diemba’, ‘Zenga Luketo’ na ‘Nokia Mubi’.

0713331200.

1200 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!