Zinedine Zidane amesema anaachia ngazi Real Madrid siku tano baada ya kuwaongoza kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Zidane aliambia mkutano na vyombo vya habari kwamba kila kitu kinabadilika na kwamba hiyo ndio sababu ya uamuzi wake

Anaondoka baada ya kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji matatu ya klabu bingwa na taji moja la ligi ya La Liga tangu achukue hatamu mnamo mwezi Januari 2016.

”Naipenda klabu hii”, aliongezea.

”Kile ninachofikiria ni kwamba timu hii inafaa kuendelea kushinda ,lakini nadhani inahitaji mabadiliko , sauti mpya, mbinu mpya. Na hiyo ndio sababu ilionisukuma kufanya uamuzi huu”.

Zidane, 45, alichukua uongozi wa klabu hiyo baada ya Rafael Benitez kufutwa kazi na alisimamia mechi 149 games.

Aliisaidia Real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia 69.8% ya ushindi mbali na mataji tisa.

Alisema mnamo mwezi Januari kwamba ataondoka katika klabu hiyo atakapohisi kwamba hana la ziada kuisaidia timu hiyo.

Hatahivyo , tangazo linaonekana kuwashangaza wengi kwa kuwa linajiri siku chache tu baada ya Real kuishinda Liverpool 3-1 katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya

“Hii ni klabu ambayo imeshinda mataji 13 ya Ulaya , kwa hivyo nafurahia kuwa miongoni mwa historia yake”, alisema baada ya ushindi mjini kiev.

Tutafikiria kuhusu kile tulichofanikiwa kufanya. Tufurahie. Huu ndio wakati muhimu zaidi.

Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino amehusishwa na klabu ya Real siku za hapo nyuma. Raia huyo wa Argentina hatahivyo aliweka kandarasi ya miaka mitano na Spurs wiki iliopita.

Mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri huenda pia akahusishwa kujaza pengo hilo , huku Arsene Wenger akitaka kuendelea na ukufunzi baada ya kuondoka Arsenal baada ya miaka 22.

Mkufunzi raia wa Itali Maurizio Sorri wa klabu ya Napoli pia anapatikana. Uamuzi wa ni nani atakayesimamia Real Madrid utatolewa na rais wa klabu hiyo Florentino Perez.

Aliandamana na Zidane katika mkutano huo na vyombo vya habari na kusema kuwa angependelea kumshinikiza mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 1998 kusalia katika klabu hiyo.

“Huu ni uamuzi ambao hatukuutarajia. Zidane aliniambia kuhusu uamuzi wake jana”, aliongezea Perez.

Kuondoka kwa Zidane kunajiri baada ya Gareth Bale na Christiano Ronaldo kufichua kwamba wanafikiria hatma yao katika klabu hiyo.

Mshambuliaji wa Wales, Bale hakufurahia kushiriki katika mechi ya fainali ya vilabu bingwa dhidi ya Liverpool kama mchezaji wa ziada huku Ronaldo akisema baada ya mechi hio kwamba atafanya uamuzi kuhusu hatma yake.

Alipoulizwa iwapo uamuzi wake unatokana na Ronaldo, Zidane alisema: Real inatafuta meneja wake wa tano katika kipindi cha miaka mitano.

1158 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!