Kiongozi Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwaonesha wanachi kitabu cha ialani ya chama chao, kwenye Mkutano huo, Morogoro
Kiongozi Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akizungumza na Wananchi wa Morogoro kwenye mkutanao

Kiongozi Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro baada ya kukosa dhamana.

Kiongozi huyo anashikiliwa tangu jana alipokamatwa kwa kufanya mkusanyiko bila kibali. Zitto alikamatwa katika Kata ya Kikeo iliyopo wilayani Mvomero na alitarajiwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dakawa lakini akahamishiwa Morogoro Mjini.

Tangu jana saa 4:42 mpaka saa 5:40 usiku, alikuwa akitoa na kuandika maelezo ya kosa analotuhumiwa kulitenda akiwa na wakili wake, Emmanuel Mvula.

Wakili huyo amesema licha ya kukamilika kwa utaratibu huo, Polisi wamezuia dhamana ya mteja wake wakisubiri maelekezo kutoka juu.

“Polisi wanekataa kusema kama dhamana yake ipo wazi na kutaja masharti yake. Pia hawajaeleza iwapo watamfikisha mahakamani kesho (leo) kwa mujibu wa sheria,” alisema Mvula.

Tangu Februari 19; Zitto pamoja na viongozi wenzake waandamizi wa chama hicho wapo kwenye ziara ya kuitembelea mikoa minane yenye kata zinazoongozwa na ACT Wazalendo ili kuwashukuru kwa kuwachagua wawakilishi hao, kushiriki kazi za maendeleo na kuzungumza na kamati ya maendeleo ya kata hizo.

By Jamhuri