MMILIKI wa mabasi ya ‘Zacharia’, Peter Zacharia, anashikiliwa na vyombo vya dola mkoani Mara kwa tuhuma za kuwapiga risasi maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wakiwa katika majukumu yao.

Maofisa hao wanasemekana wako hospitali ya mjini Tarime wakipata matibabu ambapo mmiliki huyo wa mabasi anategemewa kufikishwa mahakamani wakati wowote.