Mamia ya wakazi wa Zanzibar wamefurika kwa wingi katika eneo la Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja Kwa ajili ya mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Chama Chama Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wameanza kufika kwenye viwanja hivyo saa mbili asubuhi, wakitoka maeneo mbalimbali leo Septemba 17,2025
Kadri muda unavyozidi kwenda ndiyo idadi ya mamia ya wananchi unaongezeka, huku viongozi mbalimbali wa kitaifa wakifika uwanjani hapo.
Katika mkutano huo, pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi naye anahudhuria.
