Na Kulwa Karedia, JamhuriMedia- Mbinga
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema mwitikio wa wananchi wa Wilaya ya Mbinga unaonyesha wako tayari.
“Nimevutiwa na umati mkubwa, Mbinga ina historia na mchango wa Watanzania.
Amesema mchango huo, unatoka na Rais wa awamu ya nne, Hayati Benjamin Mkapa alisoma hapo kati ya mwaka 1952-53.
“Mbinga ni sehemu muhimu sana,”amesema.
Amesema wilaya hiyo, ni kituo kizuri cha uzalishaji wa kilimo.

Amesema amekwenda kuomba kura ili kufanya kazi ambayo ameifanya miaka mitano iliyopita.
Amesema anakwenda kwa kujiamini mno kwa sababu amefanya mambo makubwa, hivyo ana uhakika mambo yatakuwa safi.
Amesema kwenye sekta za afya, umeme na maji wanakwenda kukamilisha kila kitu.
Amesema wametekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2025 vizuri na sasa wanageukia vitongoji.
Kuhusu usambazaji wa maji wanakaribia asilimia 90 kitaifa.
Amesema Mbinga Vijijini kuna miradi 21 ambayo inaendelea vizuri, hatua hiyo itafanya kila mwananchi kupata maji.

Kuhusu afya na elimu,amesema itakuwa ni kazi ya kila awamu inayoingia kwa sababu idadi ya watu inaongezeka kila wakati.
“Kazi ya elimu na afya niendelevu, tuendelee kufanya kazi ili watoto wetu wapate elimu .
Kuhusu kilimo,mesema wilaya Mbinga imeongoza kwa kuongeza mazao ya kilimo na kusisitiza Serikali itaendelea kutoa ruzuku ya mbolea.
Amesema wana mpango wa kutumia vijana wanaopata maalumu kupitia mpango wa BBT Ogani ambao unasaidia kutoa elimu kwa wakulima.
Amesema ahadi yake kubwa kwa wananchi ni kuhakikisha Serikali inatafuta masoko bora ili wakulima wafaidike na shughuli za kilimo chao.

Kuhusu barabara amesema zinakwenda kujengwa ili zipitike wakati wote iwe jua au mvua kwa mwaka mzima.
Amesema serikali inakwenda kujenga daraja la mtoto Lumeme ili kupunguza matatizo wanayokutana nayo wananchi.
“Nawaomba sana Serikali iko nanyi, ahadi yetu ni kuwatumikia, mkitupa ridhaa yenu tunakwenda kufanya kazi, tunakwenda kujali utu wa kila mtu, bila kujali rangi wala nini.
“Pamoja na kusema hayo yote, hivi huko nyuma mtaacha CCM ishindwe kweli,”alihoji.
