Na Mwandishi Wetu ,JamhuriMedia,
Dar es Salaam
Hospitali zote hazina budi kuanzishwa kwa huduma za Kifamasia Tabibu katika Hospitali kuanzia ngazi ya Rufaa Kanda,Mikoa hadi vituo cha afya
Ameyasema hayo Septemba 25, 2025 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubungo Mhimbili Moi Dkt Mpoki Ulisubisya katika hafla ya Sherehe ya Maadhimisho ya Wafamasia Duniani iliyobeba kauli mbiu isemayao ‘Tukifikiria Afya Tufikirie na Famasia’
” Kauli hii imekuja katika wakati sahihi kuikumbusha jamii ya wafamasia juu ya jukumu kubwa lililowekwa juu ya mabega yao kuhakikisha afya za Watanzania wote zinalindwa wakati wote kwa kuzingatia umuhimu wa Wafamasia katika kutoa huduma kwa Wagonjwa ” amesema Mpoki.

Amesema wameona tija ya Mfamasia kuwa sehemu ya matibabu ya mgonjwa hivyo Wizara inaendelea kuajiri wafamasia katika huduma za Afya na kutoa ufadhili wa masomo ya ubobezi na kutambua ubobezi wao ili kuongeza ya Wafamasia wengi zaidi katika Sekta hiyo.
Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Famasia, Boniface Magige amesisitiza ili wapatikane Sekta inayohudumia Jamii bila kujali Sekta ya Umma au binafsi lazima kupanua wigo wa huduma katika jamii na kadri wigo wa huduma za kijamii unavyoongezeka ndivyo ajira zinavyoongezeka zaidi.
Hata hivyo amesema katika kuimarisha afya ya jamii na sunia kiujumla eneo la figo ni tatizo kwa jamii hivyo linahitaji Wafamasia wabobee katika eneo hilo ili kuhudumia wagonjwa kwa karibu zaidi.

” Tunaamini huko tunapoelekea katika masuala ya figo, moyo na tumbo wabobezi watakaokuja watafanya kazi nzuri na Jamii itatambua kwa ujumla kazi ya Mfamasia kwani tunajua ukuaji wa taaluma hii unakua kwa kasi”a mesema Msajili.
Aidha takwimu za sasa zinaonyesha kuwa Wafamasia wamefikia idadi ya 4123 nchi mzima na bado wapi wengine wanafanyia wafunzo ya utarajali na wanatarajia kuhitimu hivyo wataongezeka hivyo lazima wajipange kuongeza huduma kwa jamii.
Aidha wito umetolewa kwa Wafamasia kuwa milango ya fursa inafinguka na katika maisha ukitaka kufanikiwa vita unaianzisha mwenyewe halafu wale watakaokuona unapambana watakuongezea nguvu kwa kuwa fursa zinafunguka kadri unavyotoa huduma hivyo Wafamasia wajitokeze kwa wingi kujiendeleza kielimu ndani na nje ya nchi.




