Na Kulwa Karedia, Jamhuri Media-Kibaha

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema endapo akichaguliwa kuongoza atahakikisha anajenga bandari ya Bagamoyo.


Akizungumza na maelefu ya wananchi wa Mkoa wa Pwani kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Kibaha wakati wa kampeni za uchaguzi Septemba 28, 20205, Rais Samia amesema ujenzi huo umesubiriwa muda mrefu.


Ujenzi huu umesubiriwa mwa muda mrefu mno, mkitupa ridhaa tunakwenda kuijenga bandari hii katika eneo la Mbegani, itakuwa na gati za kisasa na ndefu, itakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa zaidi za mizigo kama bandari ya Dar es Salaam.


Bandari hii pia itaungwanishwa kwa reli ya kisasa (SGR) kwa kipande cha kilomita 100 kutoka bandari kavu ya Kwala hadi bagamoyo. Itajengwa sambamba na eneo maalumu la uchumi lenye ukubwa wa hekta 9,800 zitakazpchochea uzalishaji na kuvutia uwekezaji wa viwanda,amesema.


Amesema mpaka sasa wamekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi wa bandari na eneo la biashara.


tunakwenda kutengeneza mradi huu kupitia Mamlaka ya Bandari Tanznaia (TPA), Shirika la Reli Tanzania (TRC) na sekta binafsi hususani kwenye kongani za viwanda, amesema.


Amesema miradi hiyo ni ya kimapinduzi zaidi ambayo inakwenda kufanyika ndani ya mkoa huo na kuufanya kuwa kitovu cha usafirishaji na kuongeza fursa za ajira na biashara.


Amesema lengo kuu la serikali ni kusimamia na kuendeleza miradi hiyo muhimu kwa manendeleo na nchi kwa ujumla. Mkoa huu unastahili pongezi za pekee kwa kazi kubwa ya maendeleo ya viwanda, kumekuwa na ongezeko la viwanda 1,587 mwaka 2020 hadi viwanda 1631, hii ni sawa na ongezeko la viwanda 234 ndani ya miaka minne au viwanda 61 kila mwaka.


Katika kipindi hiki, viwanda vikubwa 97 vimejengwa na jumla vipo 156 ni sawa na ongezeko la viwanda 17 vinajengwa kila mwaka, viwanda vya kati 81 vimejengwa na sasa vipo 191 sawa na viwanda 27 kila mwaka vinajengwa,amesema.


Amesema viwanda hivyo vimetoa ajira za moja kwa moja 22,149 na zisizo za moja kwa moja ni 60,000.


Uwekezaji unaofanyika Pwania na kote nchini uwezesha nchi kupiga hatua kubwa katika mwelekeo wa kujitegemea kipato, lakini kibiashara. Sasa kuna uzalishaji mkubwa unaotufanya tujitegemee kwenye bidhaa kama vioo,malumalu, saruji, mabati ya rangi, haya ni machache kati ya mengi.


Kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa viwanda na kufanikisha ufanisi, tumeamua kujenga vituo vya kupoza umeme pale Msufuni (Mkuranga) kwa gharama ya Sh milioni 388.6 na Segerea milioni bilioni 54.7 na Zianga Sh bilioni 120 Bagamoyo,:amesema.


Amesema hatua itasaidia kuwa na umeme wa uhakika na kufanya mkoa hup kutokuwa na upungufu wa umeme.


Amesema kutokana na mafanikio hayo, serikali imejipanga kujenga mtandao wa gesi mpaka Chalinze ambao utakuwa na matoleo kwenye maeneo ya uwekezaji kama TAMCo, kwenye reli na Bagamoyo.


Mkandarasi mshauri anaendelea na tathimini ya kazi ya kupitisha bomba la gesi na ujio huu utasaidia kuvutia wawekezaji mkoani humu kwa sababu viwanda vinaweza kuendeshwa kwa gharama nafuu na bidhaa zinazozalishwa zitapungua bei yake.


Miongoni mwa ahadi zetu kwenye Ilani ni kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi nchini ili kuwezesha wananchi hasa wa kipato cha chini kuweza kujenga nyumba bora na za kisasa na gharama nafuu, mwelekeo wa serikali ni kuendelea na mpango wa ujenzi wa makazi bora na bei nafuu. Mkoa huu umekuwa wa mfano katika kuibeba ajenda hii,amesema.


Amesema serikali itaendelea kuboresha makazi mijini kuhakikisha nyumba na majengo yanarasimishwa kwa kupimwa na kumilikishwa.


Kuhusu suala maji, Rais Samia amesema serikali ilitenga zaidi ya Sh bilioni 187.3 kwenye mkoa huo kitendo ambacho kimesaidia kukamilisha mradi wa maji safi na salama kutoka asimilia 67 mpaka 89.


Natambua bado kuna maeneo yanachangamoto ya maji, kazi inaendeleea, tunakokwenda mbele tutakamilisha miradi mingine minne yenye thamani ya shilingi bilioni 44 ambayo inaendelea tunakwenda kukamilisha.


Mradi wa maji Rufiji tunakwenda kukamilisha na kata 53, Kibiti, Mkuranga na Kisarawe, ikikamilika, mradi wa Mkuranga utanufaisha maeneo ya Kwala na maeneo ya viwanda,amesema.


Amesema watajemga mradi wa maji katika eneo la viwanda wilayani Bagamoyo ambao utagharibu Sh bilioni 10.9.


Kwa upande wa sekta ya afya, amesema wamefanya maboresho makubwa ya hospitali ya mkoa huo Tumbi ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo cha kusafirisha damu, vifaa tiba mbalimbali vikiwamo CT SCAN.


Kazi kubwa tumeifanya hapa, tunafikiria kuweka MRI Tumbi ili wananchi wapate matibabu kwa wakati badala ya kwenda kupata tiba.


Mbali na hayo, tumewekaza kwenye miundombi ya umeme, tutajenga kituo kipya cha kupoza umeme kutoka bwawa la Mwalimu Julius Nyerere na kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa. Pia tunajenga njia mpya ya KV 400 kutoka Chalinde-Kinyerezi hadi Mkuranga, nawahakikishia mradi hu utapunguza tatizo la umeme.amesema.


Amesema anatmbua umuhimu wa kuwapo mahitaji ya barabara kutokana na msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro kutokana na wembemba wa njia hiyo.


Tayari usanifu unaendelea, barabara kutoka Maili moja hadi Picha ya Ndege ili iwe na njia sita za magari na njia mbili za BRT, tutaboresha mtandao wa barabara wenye urefu kilomita 71, ukamilishaji wake utaboresha huduma kwa wananchi.


Kwa kushirikisha sekta binafsi kuingia ubia tutatekeleza ujenzi wa barabara ya haraka kibaha-Chalinze- Morogoro inajengwa kwa awamu, tukiamini fedha za serikali zinasaidia huduma ya jamii na zinarudishwa,kazi imeanza.