Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Pwani

Mgombea urais wa ChamaCha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga Oktoba 29, mwaka huu kwa sababu kuna usalama upo wa wa kutosha.


Amesema kutokana na mahudhurio mazuri ya wafuasi wa chama hicho, ana uhakika siku hiyo watajitokeza hivyo hivyo.


Rais Samia amesema hayo Septemba 28 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msoga wilayani Chalinze akiwa njiani kwenda mkoani Tanga.


“Nawaomba endeleeni kuiamini CCM ipigieni kura kwenye nafasi ya Rais, wabunge na madiwani.


“Msiwe na wasiwasi nawatoa hofu siku hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa, viko imara kinachotakiwa ni kwenda kwa wingi kupiga kura na kurudi nyumbani.
Mwisho

Ameyasema hayo leo tarehe 28 Septemba 2025 kwenye mikutano yake ya kampeni hizo za Urais akiwa mkoani Pwani.