Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema atajenga uwanja wa kisasa wa michezo katika eneo la Msoga wilayani Chalinze mkoani Pwani kama atashinda uchaguzi mkuu.
Rais Samia ametoa kauli hiyo, leo Septemba 28, 2025 aliposimama kuzungumza na wananchi wa eneo wakati wa mkutano wa kampeni akiwa njiani kwenda mkoani Tanga.
Nitafanya hivi kama shukrani yetu kwa kazi nzuri ya utumishiwa Rais mstaafu Jkaya Kikwete, kuna wengi tumewapa majina yako, lakini si Msoga, eneo hili hatukufanya kitu, sasa uwanja ule tutjenga Msoga kama njia ya kuonyesha shukrani kwako.
