Wananchi wa Tanga Mjini walijitokeza kwa wingi kushiriki mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika tarehe 29 Septemba 2025. Katika mkutano huo, mgombea wa urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, aliwasilisha na kunadi Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho, akiwahimiza wananchi kuichagua CCM kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.







