Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia,Pwani

Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imewataka wawekwzaji wazawa na wakigeni kwenda kuwekeza katika eneo kongani la viwanda Kwala mkoani Pwani.

Rai hiyo imetolewa na kaimu meneja mawasiliano kwa umma na habari Adelina Rushekya wakati wa ziara ya kutembelea eneo hilo Kwa ajili ya kulitangaza kwa wawekezzaji .

Adelina amesema ziara hiyo ni mwendelezo baada ya uzinduzi wa tarehe 12 Septemba kuzindua maeneo manne ya kimkakakati ya kiuchumi.

Kaimu meneja mawasiliano Adelina Rushekya

Amesema eneo hilo ni zuri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali kwa sababu huduma zote muhimu za serikali zinapatikana ikiwemo TRA,TBS ,TANESCO na ofisini zingine zenye huduma muhimu zinapatikana eneo hilo.

“Uwepo wa huduma eneo moja inamrahisishia mwekezaji kupunguza, gharama za kwenda huku na kule kufuata huduma”amesema.

Amesema wao kama TISEZA ,wamewapa nafasi kubwa wawekezJi wa ndani kwenda kuwekeza eneo hilo Kwa kuwapa masharti nafuu ya mtaji ambapo mtanzania atatakiwa kulipia dola milioni 5 na mgeni dola milioni kumi kwa ajili ya kuanza uzalishaji.

‘Lengo la kufanya hivyo ni kuwahamasisha, watanzania wengi kuwekeza eneo hilo kwasababu wakifanya maendeleo yatabaki nyumbani na pesa zitabaki nyumbani “amesema.

Aidha amesema kuwekeza katika eneo hilo kutakuwa. na faida Kwa wawekezzaji wote watapewa eneo la ekali moja bure na watanufaika na misamaha mbalimbali ya kodi.

Amesema TISEZA inataka , kuendeleza maeneo ya uwekezaji Kwa ajili ya kuinua hiwanda nchini .

Amesema Kwa sasa wameanza na maeneo manne ya maalum ya kiucumi ambayo ni Bagamoyo kuna ekali 151 ,,Buzwagi ekali 1333 Nara ekali 607 na Kwala 100 kwa ajili ya masuala ya uwekezaji pia Serikali imeweka miundo mbinu thabiti Kwa ajili ya kuwapunguzia gharama.

” Tunataka viwanda viweze kuzalisha bidhaa za ndani Kwa kuchakata , badala ya kuuza nje kama malighafi.

Tunatarajia Kila mwekezaji aweze, kudhalisha ajira za moja Kwa moja 100 na eneo la kiwanda liwe limejengwa ndani ya miezi 12 “amesema

Meneja msaidizi wa kiwanda cha Sinosea ambacho kinatengeneza mafriji Gerald Thilia amesema kiwanda hicho kimeajili watanzania 30 mpaka sasa na kina uwezo wa kuzalisha friji ndogo 100

Amesema mwanzoni, kiwanda hicho kilikuwa kinasimamiwa na raia wa china katika uzalishakji lakini sasa wamebakia watanzania ndiyo wazalishaji na mchina mmoja tu amebaki katika .maswala ya utawala.

Kituo cha Kwala