Na Mwandishi Wetu,Jamhuri Media-Same
Mratibu wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM),Kanda ya Kaskazini, Frederick Sumaye amesema wananchi wa kanda hiyo wameahidi kufuta hali fulani ambayo ilikuwa inakisumbua chama hicho na mambo yatakuwa safi.
Sumaye ametoa kauli hiyo alipopewa nafasi ya kusalimilia mamia ya wananchi wa Same wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu leo Septemba 30,2025 mkoani Kilimanjaro.
“Jambo kubwa zaidi wamesema watashangaza kila mtu kwa kupiga kura nyingi.
“Katika kanda hii baadhi ya sehemu zingine hazikuwa nzuri sana kwa chama, wamesema watafuta hali hiyo,”amesema.
Amesema chama hicho
Kanda ya Kaskazini kiko vizuri na wananchi wameahidi kukipa kura nyingi kuliko Kanda zingine.
“Kama tunavyojua mikoa nayo inashinda, wilaya, tarafa zinashindana,tunakuhakikishia tuko vizuri.
“Same ndiyo wilaya ya kwanza unaingia Mkoa wa Kilimanjaro, karibu kaskazini, walisema watakupokea kwa kishindo. Huu ni mwanzo utakayoyaona mengi,wametuahidi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29.
“Kubwa zaidi watashangaza kila mtu.
Amesema hali hiyo inatokana na Rais Samia kuweka alama nyingi maeneo mbalimbali kuanzia jimbo, kijiji na kata kutatua matatizo mengi yaliyokuwa yanasibu wananchi.
