Na Kulwa Karedia, JamhuriMedia,Mwanga

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameseama serikali imetenga Sh bilioni 1.9 kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya kuondoa magugu maji Ziwa Jipe lililopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.


Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akituhubia wananchi wa wilaya hiyo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu leo Septemba 30,2025.


Tumetenga shilingi bilioni 1.9 kununua mitambo ya kuondoa magugu maji yanayotishia uhai wa ziwa lile, tunategemea mitambo mitambo hii tutaipokea ndani ya miezi michache ijayo, tutaitumia hapa Ziwa Jipe na maziwa mengine ndani ya nchi yetu,amesema.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Mwanga katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Septemba, 2025.
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Septemba, 2025.