Na Mwandishi Wetu,Jamhuri Media-Same
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesimulia namna alivyokwenda Kijiji cha Hedaru wilayani Same ambacho alikuta zahanati mbovu inatoa huduma kwa waja wazito hali iliyomsikitisha.
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wananchi wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wakati wa mkutano wa kampenzi za uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani Septemba 30, 2025.
Mwaka 2010 nilipoanza kampeni kama mgombea mwenza, kituo cha kwanza kiilikuwa hapa Same, nilikwenda Hedaru nilikuta zahanati mbovu inatoa huduma kwa wajawazito, hali niliyoiona haikunifurahisha hata kidogo, pamoja na kwamba nilikuwa mgombea mwenza, nililiweka kichwani mwangu kurekebisha hali ille kwa Tanzania nzima.
Leo namshukuru Mungu nimeweza kurekebisha hali hii, tutaendelea kujenga hospitali za wilaya, vituo vya afya vyenye zana kamili za matibabu, pia kupeleka madawa na watalaamu.
Nadhani ilikuwa ya Chalinze na Bagamoyo katika kutoa taarifa za uzazi hawana mwanamke aliyefariki dunia wakati wa kujifungua kwa mwaka mzima, hili ndilo lilikuwa lengo leto, kufa kupo tutakufa, lakini kujifungua au kuleta maisha mapya isiwe sababu, tutajitahidi kusambaza vituo vya afya, hospitali za wilaya na vitendea kazi nchi nzima,amesema.



