Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asharose Migiro, amewasili na kupokelewa na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya mnadani wilayani Karatu mkoani Arusha leo tarehe 3 Oktoba 2025 wakiwa tayari kumsubili na kumlaki Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Migiro ametoa salamu nzuri za ujio wa Dkt. Samia katika viwanja hivyo mda mchache ujao ambaye anatarajiwa kunadi Ilani ya CCM (2025/30) Sera na Ahadi zake ikiwa ni pamoja na kuomba kura.






