Tayari Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amewasili na kupokelewa na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake, Viongozi wa dini, Machifu, Wazee na maelfu ya wananchi wa Babati katika viwanja vya stendi ya zamani ya mabasi ya Babati mkoani Manyara, leo tarehe 4 Oktoba 2025.

Huu ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Urais ndani ya mkoa wa Manyara.