Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Ikiwa imesalia siku kadhaa Tanzania
kuungana na Nchi Nyingine Duniani kuadhimisha Siku ya Polio Duniani inayotarajia kufanyika Oktoba 24 Klabu ya Rotary Kampala imetoa hamasa kwa akina mama 317 kuhakikisha wanapojifungua watoto wao wanapata chanjo zote ikiwemo ya Polio wanapofikisha miezi 6 ili wawe salama.
Ameyasema hayo Oktoba 2025, rais wa Clabu ya Rotary Mikocheni Nasibu Mahinya katika Hospitili ya Rufaa Mwananyamala Dar es salaam wakati wakihamasisha wakina mama kuhudhuria kliniki mara baada ya kujifungua ili watoto wao wapatiwe chanjo zote kuwaepusha na magonjwa yanayoweza epukika ikiwemo kupooza.
“Hii ni wiki Wiki ya 8 ya Kampeni tuliyoianzisha klabu ya Rotary kujitolea kuhamasisha akinamama juu ya umuhimu wa chanjo ya Polio kwa wamama waliojifungua ili wahakikishe mara baada ya kuzaliwa watoto wanapata chanjo zote ” amesema rais Nasibu.

Sambamba na hayo amebainisha kuwa Polio ni ugonjwa hatari unayosababisha kupooza na kusabisha mtoto kashindwa kutembea hivyo amewasisitiza akinamama kuhakikisha wanafika vituo vya afya kupata chanjo kwani ni buree kabisa bila malipo.
Kwa upande wake mhamasishaji mwanafunzi kutoka Chuo cha Kampala, Kennedy Munisi amesema kundi la watoto wachanga wanaozaliwa wako hatarini kupata ugonjwa wa polio hivyo ndiyo maana Serikali inatoa chanjo bure za matone kwa watoto wachanga.
Pia ugonjwa huo unaambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na unashambulia mfumo wa hewa na chakula hivyo chafya kukohoa majimaji yakimpata mtu ambaye hujawahi kupata chanjo unaweza kumletea maambukizi.
