Mgombea ubunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola amesema nguvu ya maendeleo inayofanwa na mgombea urais wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan si nguvu ya soda.


Lugola ametoa kauli hiyo wakati akisalimia wananchi wa Jimbo la Bunda mkoani Mara wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwaani leo Oktoba 9,2025.


Amesema wapo watu wlaiodhani nguvu ya maendeleo inayopelekwa maeneo mbalimbali walidhani ni soda, la hasha matokeo yameonekana.


Amesema Rais amepeleka Sh bilioni 25.9 ambapo fedha hizo zimefanya maendeleo katika sekta mbalimbali.


Amesema sh bilioni 4 zimejenga jengo la halmashauri na limekamilika, ujenzi wa Chuo cha Mafunzo (VETA),umefikia asilimia 60.
“Pia tumejenga shule 4za sekondari ikiwamo moja ya high school Kwa ajili ya mkoa wa Mara iko Mwibara.


Amesema ujenzi wa barabara ya Kisorya-Nyamuswa imekamilika asilimia 100.
Kuhusu sekta ya afya, amesema serikali imepeleka vifaa tiba,madawa na kujengewa kituo cha afya Isangi.


Amesema kwa upande wa uvivu, wamepelekewa boti na kujengewa vizimba vya ufugaji samaki.