Chama cha ACT Wazalendo kimesema kitafanya kikao cha dharura leo usiku, kujadili ni namna gani wanachama wa chama hicho watapiga kura ya rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Hatua hiyo inatokana na maamuzi ya Mahakama Kuu Masjala ya Dodoma kuitupa kesi ya mgombea wa Urais wa chama hicho, Luhaga Mpina aliyekuwa akiipinga Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kumuondoa kwenye kinyang’angiro hicho.

Akizungumza leo, Oktoba 15, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Kipampa jimbo la Kigoma mjini, Kiongozi mstaafu wa chama hicho na mgombea wa jimbo