Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza leo Oktoba 27,2025 kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni ya chama hicho hapo kesho Oktoba 28,2025 ndani ya jiji la Mwanza.
Dkt.Samia amepokewa na Mgombea mwenza wa Urais wa chama hicho Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi,Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Stephen Wasira,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt.Asha-Rose Migiro pamoja na viongozi Waandamizi wa chama mkoa wa Mwanza.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Mwanza tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa ajili ya kufunga Kampeni za Uchaguzi za CCM tarehe 28 Oktoba, 2025 mkoani Mwanza.