“Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kahama

Kada wa chama cha Mapinduzi na Mwanasiasa mkongwe nchini Khamisi Mgeja amewatahadhalisha watanzania wasifanye makosa kufanya majaribio ya kuchagua wagombea uraisi ambao hawana uzoefu wa kiuongozi na hawajawahi kufanya kazi yeyote hata za serikali za mitaa hayo yatakuwa ni makosa ya kujitakia wenyewe.

Mgeja aliwakumbusha watanzania usia
Wa Baba wa Taifa Mwalimu nyerere
aliwahi kusema kiongozi bora wa nchi yetu
hawezi kutoka nje ya CCM bali atatoka ndani ya CCM na si mwingine ni Dk Samia Suluhu Hassan ambaye ndiyo chaguo sahihi la Watanzania.

Mgeja aliyasema hayo katika mikutano ya
kampeni kwenye maeneo mbalimbali
ya wilaya ya Nzega Tabora na wilaya ya
Kahama Shinyanga wakati akiwanadi wagombea wa ubunge wilaya ya Nzega jimbo la Nzega Hussein Bashe na Wilaya ya Kahama Mgombea Ubunge jimbo la Kahama mjini Benjamini Ngayiwa.

Akiwa wilayani Kahama kijiji cha Nyanhembe na Ufala amewaomba wananchi wa jimbo la Kahama mjini wachague CCM wampe kura za kishindo mgombea Urais Dk Samia na mbunge Benjamini Ngayiwa na Diwani Betha Daud.

Aliwaeleza Watanznia kwamba tunakila sababu na tunazo sababu ya kumuunga mkono mama yetu Dk Samia kwani kafanya
mambo mengi sana ya kimaendeleo katika
Nchi yetu kila sekta za kimaendeleo amezigusa.


Katika mafanikio makubwa sana na mifano ipo hai na inajieleza sisi tunawajibu wa kumlipa kura za heshima na kishindo
Hiyo Oktoba 29 tujitokeze kwa wingi twende tukatiki

Alisema Benjamini Ngayiwa Mgombea Ubunge bado kijana na unamuona ana ari kubwa sana ya kuwatumikia wananchi
wa jimbo la Kahama nawaomba tumuunge mkono kwa kumchagua ili afanye kazi ya kutuletea maendeleo katika Jimbo letu la Kahama.

Akiwa wilayani Nzega Jimbo la Nzega alimmiminia sifa nyingi mgombea Urais Dk. Samia Suluihu Hassani kuwa watanzania
wamelidhika na utendaji kazi wake mzuri uliotukuka kwani anabebwa na nia yake njema ya kuwatumikia Watanzania na Taifa kwa ujumla kwani ni mama muungwana Mchapa kazi mwenye maono makubwa mwadilifu mpenda maendeleo na anaupendo wa dhati na wananchi wake anaowaongoza.

Mgeja alimwelezea Dr. Samia kuwa ni mama aliyejaa imani ya utu katika nafsi yake tumpeni kura za kishindo kwani pamoja na mambo mazuri na makubwa
yakimaendeleo aliyoyafanya kwa kipindi kifupi cha miaka minne chini ya uongozi wake wa awamu ya sita sote tumeona maendeleo yameota kama uyoga lakini yajayo yanafurahisha zaidi Oktoba 29 Twendeni tukatiki.

Kuhusu mgombea ubunge wa jimbo la Nzega Hussein Bashe, Mgeja aliwapongeza wana CCM na wanaanchi wa wilaya ya Nzega
Kuendelea kumuunga Mkono Mbunge wao Hussein Bashe kwani ni chaguo sahihi kwao kwamaslahi mapana ya kimaendeleo katika
Jimbo lao la Nzega.

Mgeja aliyasema hayo katika mtaa wa uswilu kata ya Nzega mjini Mashariki wakati akimuombea kura Rais, Mbunge na Diwani
alimuelezea Bashe ni mmoja wa wabunge vijana mchapa kazi na mwenye maono makubwa na ameifanyia
mambo makubwa Jimbo la Nzega katika maendeleo isitoshe na taifa amefanya mambo makubwa sana katika Wizara ya Kilimo.


“Wananzega mnakila sababu ya kumuunga mkono na kumlinda kama mboni
Ya jicho lenu hakikisheni tarehe 29 Mwezi huu
Tunawaombeni muende mkampigie kura za heshima na kishindo iliaendelee kuwatumikia wananchi wa Nzega na Taifa kwa Ujumla’ alisema.

Kuhusu umoja na mshikamano wa Taifa Mgeja amewambia wananchi wa Nzega, Kahama na Watanzania kwa ujumla kuwa mshikamano upo imara japo kuna kikundi
cha watu wachache wanaotumika na mabwana zao toka nje ya nchi
kutaka kuleta chokochoko za uvunjifu wa amani napenda kuwahakikishieni
Hawataweza kutupalanganisha watanzania Mama yetu Rais Dr. Samia Suluhu Hassani
Yuko imara na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani umoja na mshikamano
Wa kitaifa

Mgeja amewaomba na kuwasisitiza Watanzania kuwa waendelee kuwa na imani kwamba nchi ipo mikono salama chini ya uongozi thabiti shupavu wa Rais wetu Dr. Samia nawaombeni mjitokeze kwa wingi sana muende mkapige kura Tarehe 29 bila hofu yeyote ile na wanaojidanganya kuleta chokochoko zozote zile zitakazo pelekea uvunjifu wa amani wajue hawataweza na ni sawa na kutaka kuchezea sharubu za simba.