Na Pendo Nguka, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua kifurushi kipya cha Faiba mlangoni kwako kinachojulikana kama T-Fiber Triple Hub kinachotoa huduma tatu muhimu katika kifurushi kimoja ikiwemo intaneti ya kasi kubwa, simu ya mezani na huduma ya intaneti pamoja na dakika kwa simu ya mkononi.

Huduma hii inalenga kuunganisha Watanzania wote katika mfumo wa kidijitali na kutoa urahisi wa kipekee kwa wateja.

Kifurushi hiki kinajumuisha intaneti ya kasi hadi 20 Mbps (upload na download), dakika 300 za mawasiliano ya mezani na ya simu ya mkononi, pamoja na GB 20 kwa matumizi ya simu ya mkononi.

Wateja wanaweza kufurahia huduma tatu kwa pamoja popote walipo, kupitia miundombinu imara ya TTCL.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko wa TTCL, Janeth Maeda, ameeleza kuwa dunia ya sasa inaendeshwa wa teknolojia, hivyo TTCL imewekeza kwa nguvu kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za mawasiliano zenye kasi, ubora, na gharama nafuu.

“Kupitia T-Fiber Triple Hub, tunalenga kurahisisha maisha ya Watanzania kwa kuwapa huduma zote muhimu kwa kifurushi kimoja na bili moja,” anasema Maeda.

Huduma hii inalenga familia, biashara ndogo na kubwa, pamoja na taasisi zinazohitaji mawasiliano ya uhakika na yenye thamani halisi. Kwa gharama nafuu kuanzia shilingi 70,000 kwa mwezi, wateja wa T-Fiber Triple Hub wanaweza kufurahia huduma bora na ya kisasa.

T-Fiber Triple Hub ni ishara ya mageuzi mapya katika mawasiliano ya kidijitali nchini Tanzania.

Huduma hii ni sehemu ya juhudi za shirika kuunga mkono ajenda ya serikali ya kuongeza matumizi ya TEHAMA na kuunganisha Watanzania wote katika mfumo wa kidijitali.

Kupitia kifurushi hiki wateja wanaweza kufurahia huduma za intaneti bila kikomo, simu za mezani, na dakika za simu za mkononi. Huduma hii inatoa urahisi wa kipekee kwa wateja, kwani wanaweza kufurahia huduma zote tatu kwa pamoja popote walipo.

Janeth Maeda ameeleza kuwa uzinduzi wa T-Fiber Triple Hub ni hatua muhimu katika kuimarisha mawasiliano ya kidijitali nchini Tanzania. Huduma hii itawezesha Watanzania wote kupata huduma bora na ya kisasa ya mawasiliano.

“kifurushi cha T-Fiber Triple Hub ni suluhisho kamili kwa wateja wanaohitaji huduma bora na ya kisasa ya mawasiliano,”anasema Maeda

Aidha Kwa gharama nafuu na huduma bora, wateja wanaweza kufurahia maisha bora na yenye urahisi.